May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Aswaar waanza kufunga Ramadhani

Spread the love

 

WAISLAM wenye madhehebu ya Answaar nchini Tanzania, wameanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan leo tarehe 13 Aprili 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa zinaeleza, Pamoja na maeneo mengine, mwezi umeonekana Saudi Arabia, Lebanon na Misri.

“Aprili 13, 2021 itakuwa siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramdhani,” ilieleza taarifa ya mamlaka ya kutangaza mwezi nchini Misri.

Katika nchini ya Lebanon, kiongozi mkuu wa madhehebu ya Sunni, Mufti Sheikh Abdellatif Deryan ametoa taarifa kwa Waislam wa nchi hiyo kuanza kufunga Ramadhani leo.

Baadhi ya Waislam katika nchi za Afrika, wenye msimamo wa kufunga kutokana na mwezi kuonekana sehemu yoyote duniani, wameanza funga hiyo leo.

Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ni moja ya nguzo tano zilizojenga dini ya Kiislam. Nguzo zingine ni Kumuamini Mungu Mmoja, kusimamisha swala tano, kuhiji Makka na kutoa zaka.

error: Content is protected !!