May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia atoa ujumbe wa Ramadhani

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka Waislamu wote nchini humo, kutumia kipindi hicho, kufanya toba na kuiomba nchi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ametoa ujumbe huo leo Jumanne, tarehe 13 Aprili 2021, kupitia ukurasa wake wa Twitter, ikiwa ni siku ya kwanza ya mfungo mtukufu wa Ramadhani.

“Nawatakia Waislamu wote mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.”

“Tukiwa katika kipindi hiki cha toba tusisahau kuiombea nchi yetu amani, upendo, mshikamano na utulivu ili kujenga mazingira bora zaidi kwa maendeleo na ustawi wa jamii,” amesema Rais Samia na kuongeza:

“Ramadhan Kareem wa Swaum Maqbul.”

error: Content is protected !!