KIONGOZI wa Kanisa la Uamsho la Moravian, Askofu Emmaus Mwamakula, amekieleza Chama cha ACT-Wazalendo, kuwa hakiwezi kuingia kwenye uchaguzi bila ya kupatikana Katiba mpya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar ea Salaam … (endelea).
Askofu Mwamakula ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, tarehe 29 Januari 2022, katika Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar ea Salaam.
Kiongozi huyo wa kiroho amesema kuwa, inabidi Watanzania waungane katika kutafuta katiba moya iliyofanyiwa marekebisho.
“Kuna jambo liko mbele yetu kila mmoja anaongea kwa neno lake, ACT-Wazalendo siwezi kuwaficha kwenye hili hamuwezi kuingia kwenye uchaguzi na katiba iliyopo. Kama imeshindikana kwa Maalim Seif Shariff Hamad, ambaye alikuwa hanunuliki, msifikiri ninyi mtaweza. Tuungane Watanzania wote katika kutetea kupatikana kwa katiba ambayo haijaandaliwa na mtu mmoja,” amesema Askofu Mwamakula.
Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, amemjibu Askofu Mwamakula akimtaka asiwe na wasiwasi kwani chama hicho kiko tayari kushirikiana na wadau wengine kupigania katiba mpya.
“Usiwe na wasiwasi Askofu, ni ajenda zetu na tutashirkiana na wadu wote wa mapambano ya kidemokrasia kama tulivyofanya nyakati zote,” amesema Ado.
Ado amesema kipaumbele cha ACT-Wazalendo ni kuhakikisha chaguzi zijazo zinakuwa za haki.
“ACT tulishatamka kupitia kikao kilichoita cha Halmashauri Kuu ya Chama Taifa, ajenda za tume huru ya uchaguzi na katiba mpya ni ajenda za kipaumbele kwa ACT-Wazalendo. Tumeyapa hayo kipaumbele sababu tunafahamu mazingira ya kisiasa ya nchi yetu,” amesema Ado na kuongeza:
“Uchaguzi utahitaji tume huru na kwetu sisi tumetamka mwaka 2022 utakuwa mwaka wa kupigania tume huru ya uchaguzi, hatutolala usiku na mchana ili uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 24 na Mkuu wa 2025 uwe na sifa tatu kwanza uwe huru, haki.”
Asanten act kwa kumuunga mkono lakini mnaitaji katiba mpya kwa faida gani lifahamishen taifa faida ya katiba mpya .idadi kubwa ya wanachi hata iokatiba ya zamani hawajui faida yake wala hasara yake. Maitaji ya wanachi ni mabadiliko ya maendeleo na walasio katiba mpya kama kweli mnataka katiba mpya anzeni ndani ya act katiba ya act sisi act tumeichoka