Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu Gwajima ataka kitambulisho NIDA kitumike NEC, TRA
Habari za Siasa

Askofu Gwajima ataka kitambulisho NIDA kitumike NEC, TRA

Spread the love

 

MBUNGE wa Kawe, jijini Dar es Salaam, Askofu Josephat Gwajima (CCM), ameshauri mfumo wa kitambulisho cha taifa kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), uunganishwe na mifumo ya vitambulisho vingine, ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Askofu Gwajima ametoa ushauri huo leo Jumanne, tarehe 12 Aprili 2022, akiuliza maswali bungeni jijini Dodoma.

“Je, Serikali haioni umuhimu wa kuunganisha mifumo ya kitambulisho cha mpiga kura na kitambulisho cha taifa ili kuepusha usumbufu?” amehoji Askofu Gwajima.

Katika maswali ya nyongeza, Askofu Gwajima, alihoji Serikali haioni umuhimu wa kuifanya namba ya NIDA itumike kama Namba ya Utambulisho ya Mlipa Kodi (TIN) na mita ya umeme kwa wananchi wenye nyumba.

Akijibu maswali hayo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamza Chande, Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Khamis Hamza Chande amesema NIDA na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Machi 2022, zimeanza mazungumzo ya kuuunganisha mifumo hiyo.

Josephat Gwajima, Mbunge wa Jimbo la Kawe (CCM)

“Mawasiliano kati ya taasisi hizi mbili yenye dhumuni la kuiwezesha kanzi data ya NIDA kutumika katika uboreshaji daftari la wapiga kura yameanza Machi 2022. Mazungumzo ya awali kati ya wataalamu wa taasisi zote mbili yenye nia ya kuunganisha mifumo hiyo mwili yamepangwa kufanyika kabla ya Mei 2022,” amesema Chande.

Chande amesema matarajio ya Serikali ni kuona mifumo hiyo inaunganishwa ili kuwarahisishia wananchi kushiriki katika shughuli za uchaguzi na kupunguza gharama za uandikishaji na uchapishaji vitambulisho vya kupigia kura.

Kuhusu ushauri wa namba ya NIDA kutumika kama TIN na mita ya umeme, Chande amesema “hilo jambo ni jema tunalichukua kwenda kulifanyia kazi, kwa sababu sio Tanzania tu, zipo nchi zimefanya huu mfumo zinatumia NIDA na kitambulisho kingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!