May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ahmed Ally afunguka ubora wa Fiston Mayele

Spread the love

 

MARA baada ya kuibuka mjadala kwenye mitandao ya kijamii juu ya ubora wa mshambuliaji wa klabu Yanga Fiston Mayele, Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amesema kuwa mchezaji huyo anakitu ndani yake kinachomfanya kuwa bora na kujitofautisha na wengine. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Ahmed aliyasema hayo kwenye moja ya kipindi cha uchambuzi wa Magezeti, hii leo tarehe 12 Aprili 2022, wakati wakipitia kurasa mbalimbali za michezo kwenye magazeti hayo.

Katika mjadala huo Ahmed alisema kuwa, mpira wa miguu ni mchezo wa namba, na mpaka sasa mshambuliaji huyo ameshapachika jumla ya mabao 11 na kwenye Ligi Kuu kunawashambuliaji ambao wamecheza mismu mitano na hawajafikisha idadi hiyo ya mabao.

“Mpira ni mchezao wa namba anamagoli 11 ndio kinara ukisema sio bora inabidi ututajie bora.”

“Kuna washambuliaji wengi wanacheza hii Ligi kwa msimu mitano au minne, hawajawahi kufikisha mabao 10 kwa hiyo ana kitu unaweza kumpongeza kwa kile kitu ambacho anacho.” Alisema Ahmed

Mjadala juu ya ubora wa mshambuliaji huyo uliibuliwa hivi karibuni na msemaji wa klabu ya Azam FC, Thabiti Zakaria maarufu kama Zaka za Kazi, mara baada ya kunukuliwa akisema kuwa mchezaji huyo ni wakawaida sana tofauti na watu wanavyomsifia.

Mpaka sasa kwenye Ligi Kuu Tanzania mara baada ya kupigwa kwa michezo 19, mshambuliaji huyo raia wa kidemokrasia ya Congo, ameshapachika jumla ya mabao 11na kumfanya kuwa kinara kwenye msimamo wa wafungaji.

Aidha Meneja huyo aliendelea kusema kuwa, kwa upande wake Mayele ni mchezaji mzuri kwa kuwa anakitu ndani yake na kufunga mabao 10 sio jambo dogo.

“Kwangu mimi ni mchezaji mzuri kufunga mabao 10, kwenye Ligi aliyocheza kwa mara ya kwanza si jambo dogo, anakitu ndani yake ambacho anacho.” Alisema Meneja habari huyo

Mshambuliaji huyo alisajiliwa na Yanga kwenye diorisha kubwa la usajili kwa mkataba wa miaka miwili, akitokea kwenye klabu ya AS Vita inayoshiriki ligi Kuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku ukiwa ni msimu wake wa kwanza kukipiga ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

error: Content is protected !!