Tuesday , 26 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Askofu Dk. Alex Malasusa mkuu wa KKKT mpya mteule
Habari MchanganyikoTangulizi

Askofu Dk. Alex Malasusa mkuu wa KKKT mpya mteule

Spread the love

Wajumbe wa Mkutano Mkuu 21 wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wamemchagua Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dk. Alex Malasusa kuwa Mkuu wa Kanisa kuchukua nafasi ya Askofu Dk. Fredrick Shoo ambaye amemaliza muda wake kikatiba. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Mwenyekiti wa uchaguzi huo, Askofu Amon Mwenda amesema Askofu Malasusa amechaguliwa jana Alhamisi baada ya kupata kura 142 akifuatiwa na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Dk. Abednego Keshomshahara aliyepata kura 96 za Wajumbe wa Mkutano.

Askofu Malasusa amechaguliwa kwa mara ya nyingine ambapo alitumikia nafasi hiyo kuanzia mwaka 2007 kabla ya kuikabidhi kwa Askofu Dk. Fredrick Shoo mwaka 2015. Kwa mujibu wa Katiba ya Kanisa haizuii Askofu aliyewahi kuwa Mkuu wa Kanisa kuchaguliwa tena.

Askofu Malasusa alizaliwa tarehe 18 April, 1961 katika kijiji cha Kiwira Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Ni mtoto wa pili katika familia ya watoto nane ya Marehemu Mchungaji Gehaz Japhet Malasusa na Subilaga Timoth Malasusa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia apewa tano ujenzi barabara Mtwara

Spread the loveWANANCHI wa Mkoa wa Mtwara, wameishukuru Serikali ya Rais Dk....

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kununua mitambo 15 ya kuchoronga miamba

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Madini imepanga kununua mitambo 15 ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Mtanzania aweka rekodi kimataifa kwa kiwanda cha kusafisha dhahabu

Spread the loveIMEELEZWA kuwa Kiwanda cha Kusafisha dhahabu cha Geita Gold Refinery...

error: Content is protected !!