Rais Mstaafu wa Marekani, Donald Trump jana Alhamisi amejisalimisha kwa Polisi katika Jimbo la Georgia kutokana na mashtaka yanayomkabili akidaiwa kujaribu kubadili matokeo ya uchaguzi kwenye jimbo hilo mwaka 2020. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).
Hata hivyo, Trump ameachiwa kwa dhamana baada ya kulipa Sh 500 milioni, ambapo sasa anasubiri kufikishwa mahakamani.
Trump ambaye anawania kugombea tena Urais wa Marekani katika uchaguzi ujao amesema kesi hiyo ni janga kwa haki, na kwamba mashtaka hayo ni ya kisiasa yanatokana na ukweli kwamba anaonekana tishio kwa Rais Joe Biden.
Jeshi la Polisi nchini humo limetoa picha ya Trump aliyopigwa baada ya kukamatwa kama inavyofanyika kwa watuhumiwa wengine ambapo namba aliyopewa ni P01135809.
Trump ameshtakiwa pamoja na watuhumiwa wengine 18 wakidaiwa kuwa walijaribu kuingilia matokeo ya uchaguzi katika jimbo hilo kufuatia kushindwa na mpinzani wake Joe Biden.
Alinaswa kwenye sauti ya simu akimuamuru msimamizi mkuu wa uchugazi katika jimbo hilo kutafuta kura 11,780 wakati wa kuhesabu kura, idadi ambayo ingempa ushindi.
Leave a comment