Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu Bagonza amzungumzia Mbowe, Urio na ACP Kingai
Habari za Siasa

Askofu Bagonza amzungumzia Mbowe, Urio na ACP Kingai

Spread the love

ASKOFU wa Dayosisi ya Karagwe ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, KKKT, Dk. Benson Bagonza, amesema juhudi zinahitajika ili kuijenga Tanzania mpya yenye umoja na mshikamano, ambayo wapinzani wataishi pamoja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa…(endelea).

Askofu Bagonza ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, tarehe 8 Machi 2022, mkoani Iringa, akizungumza katika kongamano la maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, lililoandaliwa na Baraza la Wanawake la Chadema (BAWACHA).

Kiongozi huyo wa kidini, amesema nchi inatakiwa ifikie hatua ya mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amuoe mwanachana wa Chadema, bila ya kufikiriwa kwamba anasaliti itikadi yake.

Katika kutolea mfano huo, Askofu Bagonza amesema inatakiwa ifikie hatua Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Ramadhan Kingai, amualike Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kwenye sherehe ya kumuaga ‘Send Off’, mtoto wake.

Pia, Askofu Bagonza amesema, inatakiwa ifikie hatua mtoto wa Luteni Denis Urio, amuoe mtoto wa Wakili Peter Kibatala.

“Nisisitize, Tanzania mpya ni yetu sote, mpaka tufikie hatua ambayo MwanaCCM amuoe mwana Chadema, bila kufikiriwa kwamba anasaliti. Afande Kingai amualike Mbowe kwenye send off ya mwanawe. Tanzania ambamo mtoto wa Denis Urio, amuoe mtoto wa Kibatala na iwe furaha na kucheza,” amesema Askofu Bagonza.

ACP Kingai alikuwa mpelelezi mkuu wa kesi ya uhujumu uchumi namba 16/2021, iliyokuwa inamkabili Mbowe na walinzi wake, Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya, kwenye Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam.

Wakati Luteni Urio akiwa mtoa taarifa ya mipango iliyodaiwa kusukwa na Mbowe, ya kutekeleza vitendo vya ugaidi, huku Wakili Kibatala akiwa Kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Utetezi , kwenye kesi hiyo iliyokuwa na mashtaka matano ya ugaidi.

Katika kesi hiyo iliyoondolewa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu, tarehe 4 Machi 2022, Mbowe na wenzake, walidaiwa kupanga njama za kutaka kuwadhuru viongozi wa Serikali, kufanya maandamano nchi nzima na kulipua vituo vya mafuta na maeneo yenye mikusanyiko ya watu.

Kesi hiyo ilikuwa inasikilizwa mahakamani hapo, mbele ya Jaji Joachim Tiganga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yatoa kauli wanaolala nje Hospitali ya Muhimbili

Spread the loveSERIKALI imesema inajipanga kushirikiana na sekta binafsi kujenga majengo yatakayosaidia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara yaomba bajeti ya Sh. 67.9 bilioni, wamachinga watengewa bilioni 10

Spread the loveBAJETI ya Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yahamasisha uanzishaji vituo vya kulea watoto wachanga

Spread the loveSERIKALI imewahimiza wananchi kujenga vituo vya kulelea watoto wadogo na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

error: Content is protected !!