Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Askofu Bagonza ajitosa mgogoro Konde
Habari Mchanganyiko

Askofu Bagonza ajitosa mgogoro Konde

Spread the love

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe Dk. Benson Bagonza ametaka tofauti zilizopo baina ya Askofu wa Doyosisi ya Konde, Dk. Edward Mwaikali na Kiongozi Mkuu wa kanisa hilo, Dk. Fredirick Shoo umalizike. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya …(endelea).

Hatua hiyo imekuja kufuatia kuwapo kwa mgogoro wa kuhamisha makao makuu ya dayosisi hiyo kutoka Tukuyu kwenda Mbeya mjini, jambo ambalo halikubaliwi na viongozi wengine.

Bagonza amesema hayo katika Usharika wa Ruanda Mbeya yalipo Makao Makuu mapya ya Dayosisi Konde, ambapo alialikwa kwa lengo la kutoa elimu na kujadili barua ya Dk Shoo ya Machi 11 aliyoelekeza kwa waumini ya kuwataarifu juu ya kuwapo kwa mkutano mkuu wa dharula dayosisi ya Konde utakaofanyika Machi 22 katika usharika wa Uyole Jijini Mbeya.

Aidha, katika barua hiyo inaeleza kuwa uamuzi wa kuitisha mkutano mkuu ni kutokana ya kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo Dk Mwaikali kuendelea kukaidi makubaliano ya kurejesha makao Makuu ya Dayosis Mjini Tukuyu.

Kutokana na barua hiyo Askofu Dk Mwaikali aliamua kukutana na wachungaji pamoja na Halmashauri Kuu ya Dayosisi ya Konde kwa ajili ya kuijadili barua hiyo ambapo baadhi ya maaskofu wastaafu walialikwa.

Akichangia katika katika kikao hicho Askofu Dk. Bagonza amesema migogoro huwa na pande mbili hivyo kabla ya kulitatua tatizo la kuhamishwa dayosisi kuna haja viongozi hao kwanza kufanya upatanisho.

“Mbali na upatanisho wa viongozi hao wawili pia upatanisho wa pili ni kati ya Wanakonde wenyewe ambao kuna pande mbili zinasigana hadi kuhatarisha maisha ya waumini wao hasa baada ya uamuzi wa kuihamisha dayosisi,” alisema.

Dk. Bagonza amesema upatanisho wa tatu unapaswa kufanyika kati ya Dayosisi ya Konde na KKKT yenyewe kwani mgogoro umelichafua kanisa huku akiomba Serikali kukaa pembeni kwani mgogoro utatatuliwa na kanisa lenyewe kwani uzoefu unaonyeasha kanisa hilo halikuwai kushindwa kutatua migogoro yake.

“Mgogoro huu unapaswa kuisha na hatua ya kwanza ni kufanya upatanisho kwanza Dk. Mwaikali na Mkuu wa Kanisa Dk. Shoo wakutanishwe na mjuzi wa kutatua migogoro na hili la halmashauri kuu linaenda kuisha na kanisa litasimama,” amesema Dk. Bagonza.

Aidha, katika hatua ny

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!