October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Amuua mama yake akimdai Sh. 300,000

Spread the love

HELMAN John, anadaiwa kumuuwa kwa kumpiga na mpini wa jembe mama yake, Celina William, akimdai fedha kiasi cha Sh. 300,000. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma…(endelea).

Taarifa hiyo ilitolewa jana tarehe 1 Februari 2022 na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma, ACP James Manyama, akizungumza na wanahabari mkoani humo.

ACP Manyama alisema tukio hilo lilitokea tarehe 5 Januari 2022 katika Kijiji cha Kinonko wilayani Kakonko.

Katika tukio la mauaji lilitokea Kwilayani Kakonko, ACP Manyama alisema lilitokea tarehe 5 Januari 2022 kwneye Kijiji cha Kinonko, Celina William (63), aliuawa baada ya kujeruhiwa na mpini wa jembe na mtoto wake aitwaye Helman John ambaye alikuwa akimdi ma a yake kiasi cha Sh. 300,000.

“Mnamo tarehe 5 Januari 2022 huko Kijiji cha Kinonko, Celina William aliuawa baada ya kujeruhiwa na mpini wa jembe na mtoto wake aitwaye Helman John, ambaye alikuwa akimdai mama yake fedha kiasi cha Sh. 300,000,” alisema ACP Manyama.

ACP manyama alisema John naye aliuawa na wananchi wenye hasira kali, baada ya kutaka kumjeruhi mtu mwingine kwa shoka.

“Kitendo chake cha kukimbilia Wilaya ya Kasulu ambako aliuawa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi, baada ya kutaka kumjeruhi mtu mwingine kwa shoka eneo la Sofia,” alisema ACP Manyama.

error: Content is protected !!