May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ally Mayay akubali yaishe

Ally Mayay

Spread the love

 

ALIYEKUWA mgombea wa nafasi ya Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ally Mayay Tembele ameonesha kutokuwa na mpango wa kukauta rufaa baada ya kuenguliwa kwenye kinyang’anyiro hiko. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Ally Mayay ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania, aliondolewa kwenye kinyang’anyiro hiko siku ya jana na Kamati ya Uchaguzi ya TFF, inayoongozwa na Wakili Kiomoni Kibamba baada ya kutokizi vigezo vya kikanuni.

Baada ya kuondolewa kwenye kinyang’anyiro hiko, Mayay alisema kuwa hana mpango wa kukata rufaa na ataendelea kutoa maoni yake kama mdau na mwanafamilia ya soka.

“Watu wanasema nikate rufaa, lakini kwangu hapana mimi sio lazima kuwa kiongozi, ingawa bado ni mwanafamilia na nimehudumia mpira, nitataendelea kutoa mchango wangu kadri nitakavyokuwa hai,” alisisitiza Tembele.

Aliongezea kuwa yeye kwa sasa ataendelea kutoa maoni kama mdau wa soka kwa faida ya mpira na kusisitiza kuwa kama angefanikiwa kupita kwenye mchujo huyo, moja ya ajenda yake kwenye kampeni ni kuongeza idadi ya wajumbe kwenye mkutano mkuu, pamoja na kufanya bodi ya Ligi kuwa huru.

“Ningeongeza idadi ya wanachama hiyo ndiyo lingekuwa lengo langu kwenye kampeni kama ningepitishwa, pamoja na kuifanya bodi ya Ligi kuwa huru imilikiwe na klabu kama ilivyo kwa Uingereza, ili TFF ijikite kwenye maendeleo,” alinena Mayay.

Waliopitishwa kwenye mchujo huyo mpaka sasa ni Wallace Karia anayetea nafasi yake, Hawa Mniga pamoja na Evans Mgeusa.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa Wallace Karia alipata wadhamini 10, huku mwanamama Hawa Mniga akipata wadhamini watano na Evans Mgeusa alifanikiwa kupata wadhamini watano.

Wengine walioondolewa kwenye kinyang’anyiro hiko ni Oscra Oscar ambaye kwa mujibu wa kamati hakuwa na mdhamini hata mmoja sambamba na Ally Saleh ‘Alberto’ ambaye naye hakupata mdhamini.

error: Content is protected !!