Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Alichokisema Rais Samia baada ya kuhutubia UN
Habari za SiasaTangulizi

Alichokisema Rais Samia baada ya kuhutubia UN

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameihakikishia dunia kuwa Tanzania ni ileile yenye amani na ushirikiano na nchi zote. Anaripoti Glory Massamu, TUDARCo … (endelea).

Ametoa kauli hiyo saa chache kupita tangu amalize kuhutubia mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa New York nchini Marekani, usiku wa jana Alhamisi, tarehe 23 Septemba 2021.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia amesema “nimehutubia kwa mara ya kwanza Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.”

“Nimeihakikishia Dunia kuwa Tanzania ni ileile yenye na amani na ushirikiano na nchi zote, nimeeleza imani yangu kuwa changamoto za dunia tunaweza kuzikabili kwa pamoja ikiwemo janga la Uviko-19.”

Rais Samia ameshiriki kwa mara ya kwanza mkutano huo akiwa mkuu wa nchi, aliyeingia madarakani tarehe 19 Machi 2021 baada ya aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, kufariki dunia saa 12 jioni ya tarehe 17 Machi 2021.

Magufuli alifikwa na mauti katika Hospitali ya Mzena, iliyopo Makumbusho jijini Dar es Salaam na mwili wake kuzikwa nyumbani kwao Chato, Mkoa wa Geita tarehe 26 Machi 2021.

Katika hotuba hiyo ya Rais Samia aliyoitoa mbele ya wajumbe wa mkutano huo aligusia masuala mbalimbali ikiwemo usawa wa kijinsia, mabadiliko ya tabia ya nchi, utawala bora pamoja na mapambano dhidi ya ugonjwa wa korona.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!