October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mwandishi ITV afariki ajalini, mwenzake…

Spread the love

 

MWANDISHI wa habari wa ITV na Redio One, Mkoa wa Songwe, nchini Tanzania, Gabriel Kandonga amefariki dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Songwe … (endelea).

Kandonga amefariki dunia alfajili ya leo Ijuma, tarehe 24 Septemba 2021, katika ajali ya barabarani iliyotokea maeneo ya Karasha karibu na Shule ya Msingi Mlowo, Mbozi.

Kandonga na mwenzake wa Clouds Media, Haika Rayman walikuwa wanakwenda Mkwajuni kikazi. Haika amejaruhiwa na amelazwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Songwe.

error: Content is protected !!