Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Ajali ya moto Moro: Vifo vyaongezeka
Habari Mchanganyiko

Ajali ya moto Moro: Vifo vyaongezeka

Spread the love

MAJERUHI saba kati ya 32 waliokuwa wakiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), wamefariki dunia usiku wa kumkia leo tarehe 15 Agosti 2019. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Idadi ya majeruhi waliopokewa MNH baada ya kutokea ajali ya moto mkoani Morogoro tarehe 10 Agosti 2019, walikuwa 46 ambapo mpaka sasa hospitalini hapo majeruhi 21 wamepoteza maisha.

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 15 Agosti 2019, Meneja Uhusiano wa MNH, Aminiel Aligaisha amesema majeruhi saba wamefariki dunia kuanzia majira ya usiku hadi asubuhi ya leo.

Aligaisha ameeleza kuwa, kwa sasa majeruhi wamebakia 25 ambapo 16 kati yao wako kwenye chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) huku tisa wakiwa katika wodi ya Sewahaji.

“Tulipokea wagonjwa 46 idadi ya vifo ilikua 14 mpaka jana nilipozungumza na ninyi saa tano na nusu, nasikitika kutangaza kwamba hadi leo, wameongeza wengine 7 na kufikia idadi ya 21 mpaka sasa, kati ya wgaonjwa 46 tulipopokea wamefariki 21 na tumebaki na 25 na kati yake 16 wako ICU  na 9 wako katika wodi ya Sewahaji,” amesema Aligaisha .

Aligaisha amesema madaktari na wauguzi wanaendelea na juhudi za kuokoa maisha ya majeruhi waliobakia.

“Tunaendelea na jitihada za kutibu wagonjwa wengine. Madaktari na wauguzi wanafanya jitihada kuhakikisha majeruhi wanahudumiwa vizuri,” amesema Kebwe.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Stephen Kebwe amesema leo anatarajia kutoa idadi kamili ya vifo vya majeruhi hao, baada ya kuwepo kwa takwimu zinazotofautiana kuhusu idadi ya vifo hivyo.

Aidha, Kebwe amesema mpaka jana tarehe 14 Agosti 2019 idadi ya vifo hivyo ilikuwa 85, baada ya majeruhi wengine 14 waliolazwa MNH kufariki dunia.

Ajali hiyo ilitokea majira ya asubuhi tarehe 10 Agosti 2019 eneo la Msamvu mkoani Morogoro, baada ya tenki la lori la mafuta aina ya petrol kulipuka kufuatia baadhi ya wananchi kutoboa tenki la lori hilo na kuanza kuchota mafuta.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!