Monday , 11 December 2023
Home Habari Mchanganyiko ‘Mganga mfufuaji’ adakwa Ruvuma
Habari Mchanganyiko

‘Mganga mfufuaji’ adakwa Ruvuma

Pingu
Spread the love

DEO Mapunda, mkazi wa Ruvuma anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kutapeli wananchi kwa kujifanya mganga wa kienyeji. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizunguma na mtandao huu leo tarehe 15 Agosti 2019, Kamanda wa Jeshi la Polisi Ruvuma, Simon Marwa amesema, wamemkamata mtuhumiwa huyo baada ya wanakijiji wa Mbinga, Mhalule wilayani Songea kutoa taarifa polisi juu ya utapeli wake.

Kamanda Marwa ameeleza, Mtuhumiwa alidanganya wananchi hao ya kwamba ana uwezo wa kufufua watu waliofariki dunia, ambapo alishirikiana na kijana anayefahamika kwa jina la Abdul aliyeigiza kama amefariki na kisha kufufuliwa na Mapunda.

Amesema, baada ya mtuhumiwa huyo kuhojiwa, alikiri kufanya udanganyifu huo, huku akisema kwamba alikuwa anatangaza kazi yake ili apate wateja, huku akisistiza kwamba utapeli huo umeibuka katika kipindi ambacho wanakijiji hao wana fedha baada ya kuuza mazao yao.

“Huyo alijifanya mganga anaweza kufufua watu, alimtumia Abdul ambaye alidai amemfufua na kumuweka nyuma ya nyumba yake kwa ajili ya matangazo.

“Unajua hiki kipindi ni cha mavuno hivyo wananchi wanafedha alitaka kutumia fursa hiyo kutapeli fedha za wananchi,” amesema Kamanda Marwa.

Pia Kamanda Marwa amesema, walimkamata Raia wa Kenya, Adinikas Kyuvu aliyetuhumiwa kuwa mchungaji bandia kisha kutapeli wananchi akidai anatenda miujiza na kutatua shida za watu.

Amesema, mtuhumiwa huyo alikamtwa akiwa na kwato, kifuu cha nazi, ubani na shanga vifaa ambavyo alidai anatumia kuwaponya waumini wake.

Aidha, Kamanda Marwa amesema kwa kuwa hakuna mtu aliyelalamika kuathirika na vitendo vya mtuhumiwa huyo, Jeshi la Polisi lilimfikisha Idara ya Uhamiaji mkoani Ruvuma, ambapo idara hiyo ilimrudisha nyumbani kwao nchini Kenya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NBC yatoa msaada wa mil. 20 kwa waathirika mafuriko Hanang

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) sambamba na wafanyakazi wa...

Habari Mchanganyiko

Polisi wadaka mirungi kwenye basi la Extra Luxury

Spread the loveJeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limekamata shehena ya dawa za...

Habari Mchanganyiko

Oryx yaungana na jamii kuwafariji waathirika maporomoko Hanang

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imeungana na Watanzania kutoa pole...

Habari Mchanganyiko

Amsons Group watoa milioni 100 waathirika maafa Hanang

Spread the loveKAMPUNI ya Amsons Group kupitia kampuni zake za Camel Oil...

error: Content is protected !!