Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Shughuli pevu: Ni Lissu Vs Ndugai kortini
Habari za SiasaTangulizi

Shughuli pevu: Ni Lissu Vs Ndugai kortini

Spread the love

KESI inayotarajiwa kuwa mashuhuri na ya aina yake kati ya Tundu Lissu, aliyevuliwa ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki dhidi ya Job Ndugai, Spika wa Bunge, sasa kuunguruma. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea). 

Kesi hiyo inatarajiwa kuanza leo tarehe 15 Agosti 2019, katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam Lissu akipinga uamuzi wa Spika Ndugai kumvua ubunge.

Lissu, mmoja wanasheria mashuhuri nchini, alifungua shauri la kupinga kuvuliwa ubunge wake, kwenye mahakama hiyo Jumatano, tarehe 7 Agosti 2019, chini ya hati ya dharura.

“Maombi ya kesi hii yatasikilizwa mbele ya Jaji Mtupa. Hati ya wito wa mahakama inabainisha kuwa mlalamikiwa ambaye ni Spika Ndugai, atatakiwa kufika mahakamani bila kukosa,”

imeeleza taarifa ya Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chadema na kuongeza;

“Tunatoa wito kwa viongozi, wanachama, wafuasi wa Chadema na Watanzania wote wapenda haki, demokrasia na utawala bora unaoheshimu sheria, mahali popote walipo kufuatilia kwa karibu mwenendo wa shauri hilo kuanzia hatua ya sasa.”

Spika Ndugai alitangaza uamuzi wa kumvua ubunge Lissu, tarehe 28 Juni 2019, wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa Bunge. Hatua hiyo iliibua sintofahamu na kupingwa.

Kiongozi huyo wa Bunge, alitaja sababu za kumvua ubunge Lissu kuwa: Kushindwa  kuhudhuria vikao vya bunge bila kutoa taarifa kwa maandishi kwa spika na kutojaza fomu ya taarifa za mali na madeni kwa mujibu wa sheria ya maadili ya viongozi wa umma ya mwaka 1985.

Lissu kupitia kaka yake, Alute Mughwai, anaomba Mahakama Kuu imruhusu kufungua shauri la kupinga kuvuliwa ubunge wake, kupitia utaratibu wa Judicial Review – mapitio ya maamuzi yaliyofikiwa.

Lakini pia Lissu anaiomba mahakama itoe amri ya muda ya kusimamisha kuapishwa kwa mbunge mteule wa jimbo la Singida Mashariki (CCM), Miraji Mtaturu.

Lissu anaiomba mahakama isikilize na kutoa uamuzi wa maombi yake haraka, vinginevyo Mtaturu ataapishwa kushika wadhifa huo, na kwamba, hatua yoyote ya kutosikiliza shauri lake kwa haraka, litamuathiri moja kwa moja kwa kuwa amepoteza haki zake zote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

error: Content is protected !!