Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ado Shaibu ‘ateka’ Bunge uchaguzi EALA
Habari za Siasa

Ado Shaibu ‘ateka’ Bunge uchaguzi EALA

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, ‘ameteka’ uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, kufuatia hotuba yake na maswali aliyoulizwa na wabunge wa Bunge la Tanzania, wakati akiomba kura. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Tukio hilo limetokea leo Alhamisi, tarehe 22 Septemba 2022, wakati wagombea wa nafasi hizo walipopewa nafasi za kuomba kura kwa wabunge.

Mwanasiasa huyo wa upinzani, aliliteka bunge hilo baada ya kuwataja baadhi ya wabunge na Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, wakati akijinadi mbele ya wabunge ili wamchague.

Ado aliibua shangwe na kupigiwa makofi na wabunge wengi baada ya kujitambulisha kuwa Spika Tulia, alikuwa mkufunzi wake alipokuwa anasoma shahada ya sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Mgombea huyo wa ubunge wa EALA kupitia chama cha ACT-Wazalendo, aliwataka wabunge wamchague akisema anazifahamu sheria na kanuni za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), alizofundishwa na Mbunge wa Kilosa, Profesa Palamagamba Kabudi,  akiwa UDSM.

“Nilipokuwa UDSM nakumbuka Prof. Kabudi ambaye ni mjumbe wa bunge hili, kwa pamoja na Gastoni Kennedy, walinifundisha kozi mpya inayoitwa Sheria za Jumuiya ya Afrika Mashariki, lengo kuu ni kuwaanda mawakili wa Tanzania kama mimi, kutumikia vyombo vya EAC kama bunge, mahakama na sekretarieti,” amesema Ado.

Ado aliwaomba wabunge hao wamchangue awe mbunge wa Afrika Mashariki, akisema yeye ni muumini wa umajumui wa Afrika (Pan Africanism), huku akisema Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, Dk. Bashiru Ally, naye ni mwanachama wa falsafa hiyo.

“Dk. Bashiru anaweza kushuhudia kwamba tulifanya kazi pamoja muongo uliopita, tulijitolewa kwa pamoja katika Kigoda cha Mwalimu Nyerere, tuliimba pamoja Afrika Moja, Afrika huru,” amesema Ado.

Kufuatia kujinadi huko, wabunge kadhaa walimuuliza maswali Ado, akiwemo wa Geita Vijijini, Constantine Kanyasu, alimuuliza Tanzania ni nchi ya pili kwa ukubwa ndani ya EAC ikitanguliwa na Demokrasia ya Kongo, na kwamba ana ajenda gani kuhakikisha inaimarika katika jumuiya hiyo.

Ado amejibu swali hilo akisema “sekta kuu ya uchumi wa Tanzania ni kilimo, hivyo nitasukuma ajenda ya kutafuta masoko kwa ajili ya bidhaa za kilimo kutoka Tanzania. Jumuiya ya Afrika Mashariki ina masoko mengi. Fursa yangu ya kwanza itakuwa masoko kwa ajili ya bidhaa za kilimo,” amesema Ado.

Pia Ado aliulizwa na wabunge, kukiwa na mgongano wa maslahi kati ya Tanzania na EAC, atatetea maslahi ya upande upi, ambapo amejibu akisema “Tanzania ni nchi huru, pindi itakapotokea mgongano wa kimaslahi katika masuala ya EAC, jukumu langu ni kusimama na kutetea maslahi ya Tanzania. Ndiyo maana kauli mbiu yangu inasema nchi yangu kwanza.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!