October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Akamatwa akisafirisha kilo 158 za mirungi Arusha

Viroba vilivyosheheni bangi

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Arusha limemkamata, Benson Emmanuel (28), akisafirisha  shehena ya madawa ya kulevya aina ya mirungu yenye uzito wa kilo 158.5 katika eneo la Njiro jijini humo. Anaripoti Erick Mbawala, TUDARco…(endelea)

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo, leo tarehe 22, 2022 amesema  kuwa jeshi lilimkamata akiwa amepakia shehena hiyo ndani ya gari aina ya Rav4 yenye namba za usajili T-755 AWD Jumatano tarehe 21 Septemba, 2022 saa 3 asubuhi.

Kamanda huyo amesema pia  mtuhumiwa alikutwa na unga mweusi ndani ya gari hiyo ambao ulidaiwa kuwa ni imani za kishirikina ili asikamatwe pale atapokutana na vyombo vya usalama.

Mtuhumiwa pia amedaiwa  kuwa na  matukio kadhaa pamoja na kujihusisha na mtandao wa madawa ya kulevya katika maeneo mbalimbali.

Aidha Kamanda Masejo amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi  endapo watashuhudia tukio lolote la kihalifu katika mkoa huo na kuwaonya wale wote wanaonendelea na matukio ya kihalifu.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha tunapenda kutoa wito kwa wananchi wetu  waendelee kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za wahalifu wachache kwenye mtandao wa madawa ya kulevya,” amesema Masejo.

Aidha, ametoa onyo kwa wale wote wanaoendelea kujihusisha na madawa ya kulevya waache na wafanye biashara halali.

error: Content is protected !!