Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo yatoa mapendekezo kuboresha elimu nchini
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yatoa mapendekezo kuboresha elimu nchini

Spread the love

CHAMA cha ACT Wazalendo kimeitaka serikali kukabiliana na changamoto ya upungufu wa walimu na kuboresha elimu katika sekta hiyo. Anaripoti Rhoda Kanuti Dar es Salaam (endelea).

Hayo yamesemwa leo tarehe 11 Mei 2022 na Riziki Shahari Ngwali Msemaji wa Sekta ya Elimu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa ili kukabiliana na changamoto ya upungufu mkubwa wa walimu serikali haina budi kuajiri walimu.

Chama hicho kimesema kuwa “tatizo hilo,la upungufu wa walimu liko katika taasisi za elimu ya juu na vyuo vikuu,ambako serikali haijaweka wazi jitihada zake ili kukabiliana na mkwamo huo.”

Kwa mujibu wa taarifa za udahili wa walimu kupitia Wizara, serikali imeweza kudahili jumla ya wanafunzi wa Astashahada ya Elimu ya msingi kuwa 10,975 (wanawake 5,824 na wanaume 5,151), stashahada ya ualimu sekondari miaka miwili 2,663 (wanawake 1,037 na wanaume 1,626), stashahada ya maalum ya sekondari, sayansi miaka mitatu 5,540 (wanawake 1,973 na wanaume 3,567).

Hata hivyo hiyo imefanya vyuo vya Ualimu vya Serikali kuwa na jumla ya wanafunzi 19,178, ikiwa ni ngazi ya astashahada na stashahada pekee, pia ACT wanatoa rai kwa serikali kurejesha mfumo wa ajira za walimu za moja kwa moja ili kukabiliana na changamoto hiyo ya upungufu mkubwa wa walimu na kuboresha katika sekta ya elimu inchini.

Aidha Riziki amesema kuwa serikali haina budi kurekebisha mfumo wa elimu nchini hususani mitaala ya kwa kuwa haiendani na mazingira ya sasa.

“Wanafunzi wanaosoma shule za Englishi Medium na zile shule za kawaida serikali wanafanya mtihani mmoja ilhali wanasoma kwenye mitaala tofauti,”

Pia chama hicho kimeitaka serikali kutenganisha fedha za miradi halisi ya maendeleo na fedha kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu, kwa kuanzisha fungu maalum ili fedha za miradi halisi ya maendeleo ziweze kuonekana na kufuatilia utekelezaji wake.

Amesema katika mwaka wa fedha wa 2022/22, wizara ilipitisha bajeti ya Sh. 994.7 Bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kati ya fedha hizo bilioni 570 zilikuwa kwa ajili ya kugharamia mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, “kwa kutazama fedha hizo kwa mwaka jana fedha za mikopo zilikuwa asilimia 57 za fedha zote za miradi,”

Meongeza katika mwaka 2022/23 wizara imeomba kuidhinishwa fedha Sh 959 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo “ni fedha pungufu ukilinganisha na bajeti ya mwaka jana, hata hivyo kiasi cha gharama za mikopo kitaendelea kupanda kutokana na ongezeko la idadi ya wahitimu wa kitato cha sita kwa mwaka huu.”

Chama hicho kinaitaka serikali kuhakikisha sekta ya elimu inasimamiwa na wizara moja kwa hivi sasa imegawanywa katika wizara zaidi ya tatu, (wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ,Wizara ya Tamisemi na Wizara ya Maendeleo ya jamii,jinsia na Watoto kwa baadhi ya maswala).

“Hii imepelelea kuyumbishwa kwa mipango ya bajeti katika sekta ya elimu,” amesema Riziki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!