Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rufaa za kina Mdee zilivyosikilizwa
Habari za SiasaTangulizi

Rufaa za kina Mdee zilivyosikilizwa

Spread the love

 

BARAZA Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania limemaliza kusikiliza rufaa za Halima Mdee na wenzake 18 . Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Walianza kuingia saa 4:11 usiku wa tarehe 11 Mei 2022, katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mdee na wenzake 18 walikata rufaa kwa Baraza hilo kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho wa tarehe 27 Novemba 2022 wa kupinga kuwafukuza uanachama.

Walifukuzwa baada ya kutuhumiwa kughushi nyaraka za Chadema, usaliti na kujipeleka bungeni jijini Dodoma na kujiapisha kuwa wabunge wa viti maulum.

Utaratibu uliofanyika, alikuwa anaingia mmoja mmoja ukumbini ambapo kila walipofika, waliulizwa maelezo waliyowasilisha ya rufaa ni ya kwake na akikubali anaruhusiwa kutoka na kuingia mwingine.

Ilikuwa wakitoka kusikiliza rufaa zao, walikuwa wanaingia chumba kingine ili wasionane.

Ilikiwa inachukua kama dakika tatu hadi tano kila mmoja na ilipofika saa 5:33 usiku wote 19 walikuwa wameingia ukumbini ambapo kulikuwa na wajumbe takribani 420 wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Mbali na Mdee aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la wanawake wa Chadema (Bawacha), wengine ni, waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu, Ester Bulaya na Esther Matiko pamoja na aliyekuwa katibu mkuu wa Bawacha, Grace Tendega.

Pia wamo, Hawa Mwaifunga, aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Bawacha (Bara); Agnesta Lambat, aliyekuwa katibu mwenezi na Asia Mwadin Mohamed, aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Bawacha Zanzibar na Katibu Mkuu, Bawacha-Bara, Jesca Kishoa

Wengine ni, aliyekuwa katibu mkuu wa Baraza la Vijana (Bavicha), Nusrat Hanje, aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoani Mtwara, Tunza Malapo.

Cecilia Pareso, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Salome Makamba, Anatropia Theonest, Conchesta Lwamlaza, Felister Njau na Stella Siyao.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kujua uamuzi wa rufaa hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bunge labaini madudu mfumo ukusanyaji mapato, h’shauri tatu kikaangoni

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

Mkuu wa wilaya ya Rungwe azindua vyumba sita vya madarasa vya thamani ya 64 mil

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua vyumba...

Habari za Siasa

Mbunge afurahia mabilioni ya Samia kutua jimboni

Spread the love  MBUNGE wa Igunga, Nicholas Ngassa ameishukuru Serikali kwa utekelezaji...

Habari za Siasa

PIC yaishauri Serikali kuanzisha mfuko wa uwekezaji kusaidia mashirika ya umma

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji...

error: Content is protected !!