April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

ACT-Wazalendo yataja mmiliki wa kadi No. 1 kabla ya Maalim Seif

Maalim Seif Shariff Hamad akikabishiwa kadi alipojiunga na ACT-Wazalendo

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimeeleza kwamba, Maalim Seif Shariff Hamad amepewa kadi namba moja ili kumsahau aliyekuwa mmiliki wa kadi hiyo, Wakili Albert Msando. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea). 

Maalim Seif, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), alihamia Chama cha ACT-Wazalendo na kupewa kadi No. 1 kutokana na mgogoro wake na Prof. Lipumba, mwenyekiti wa CUF Taifa. 

Akizungumza na MwanaHALISI ONLINE, Katibu wa Itikadi na Uenezi ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema, wameamua kumpa kadi hiyo Maalim Seif ili kufuta historia ya Wakili Msando baada ya kushindwa mapambano dhidi ya CCM.

Na kwamba, Wakili Msando alinunua kadi hiyo kwa kiasi cha Sh. 1 Milioni, baada ya ACT-Wazalendo kuweka utaratibu wa kuuza kadi zenye namba kuanzia 1 hadi 1,000 kwa bei ya juu ili kuwezesha chama hicho kupata fedha kutokana na kutokuwa na vyanzo vya mapato.

“Sasa tuliweka utaratibu baada ya hiki chama chetu hakina vyanzo vya mapato , kwa hiyo tufanye ubunifu, kadi namba 1 hadi 1,000 tuziuze kwa bei ya juu, kwa hiyo kadri kadi inavyo kuwa namba 1 hadi 20 inauzwa milioni 1, na zilizofuata ni Sh. 100,000.

“Aliyenunua namba moja ni Wakili Msando, na wengine walikuwa na kadi tofauti tofauti.

“Zilizogaiwa siku ile, kadi namba moja alipewa Maalim Seif kwa sababu Msando mapamabo yamemshinda amekwenda CCM na sisi hatuwezi katika data base yetu tukabaki na Msando, tunataka kumfuta  katika ripoti zetu labda atakaa kwenye mafaili yetu kwa ajili ya kweka historia,” amesema Ado.

error: Content is protected !!