Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT Wazalendo walilia Azimio la Arusha
Habari za Siasa

ACT Wazalendo walilia Azimio la Arusha

Kutoka kushoto Esther Kyamba - Katibu wa Ngome ya Wanawake wa ACT, Ado Shaibu - Katibu wa Kamati ya Itikadi, Mawasiano ya Umma na Uenezi, Pamoja na Mohammed Babu - Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa ACT- Wazalendo.
Spread the love

CHAMA cha ACT- Wazalendo kimesema chimbuko la kiwango cha kutisha cha rushwa na ufisadi uliotamalaki nchini kwa sasa, ni uamuzi wa uongozi kufuta Azimio la Arusha, anaandika Pendo Omary.

Azimio la Arusha lilijadiliwa na kupitishwa na Halmashauri Kuu ya Chama cha TANU, iliyoketi mjini Arusha tarehe 26-29 Januari 1967 na kutangazwa rasmi siku sita baadaye – tarehe 5 Februari.

Ado Shaibu, Katibu wa itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT – Wazalendo, amesema leo hii kwamba Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana mjini Zanzibar mwaka 1992, “bila ya kuendesha mjadala wa kitaifa kwanza, iliazimia kuliua azimio hilo kwa kisingizio cha kwenda na wakati.”

“Hata misingi muhimu ya miiko ya uongozi ambayo ilikuwa sehemu muhimu ya Azimio la Arusha iliyosaidia kuhakikisha panakuwa na uadilifu katika kuongoza nayo ilizikwa,” amesema Shaibu.

Amesema chama chao kimepanga kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwa azimio hilo lililokuwa msingi mahsusi wa utekelezaji wa siasa ya ujamaa na kujitegemea chini ya uongozi wa taifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

ACT – Wazalendo kitafanya maadhimisho hayo kwa kuendesha mjadala mpana wa kitaifa tarehe 25 Machi mwaka huu jijini Arusha. “Mjadala utakuwa ni jukwaa la kitaifa kwa ajili ya kutafakari mafanikio na matatizo ya Azimio la Arusha na nafasi yake katika Tanzania ya leo,” amesema.

Kupitia Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia, mjadala utahusisha nafasi ya siasa za kijamaa na za mrengo wa kushoto barani Afrika na duniani.

Ni matarajio ya chama hicho kilicho chini ya uongozi wa Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma mjini, kwamba maadhimisho hayo yatahudhuriwa na wananchi, wanasiasa, wawakilishi wa asasi za kiraia, wanaharakati na wanazuoni kutoka ndani na nje ya nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!