Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo: Muda alioomba Rais Samia unatosha, sasa katiba mpya
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo: Muda alioomba Rais Samia unatosha, sasa katiba mpya

Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu
Spread the love

 

CHAMA cha siasa nchini Tanzania cha ACT-Wazalendo kimesema, muda ulioombwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuachwa ili kuijenga nchi kiuchumi umetosha na sasa aitishe mchakato wa Katiba pamoja na kukutana na vyama vya siasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

ACT-Wazalendo ambacho ni chama washirika wanaounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK) umesema, kikao kati ya Rais Samia na vyama vya siasa, una maslahi mapana kwa ustawi wa jamii.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu, tarehe 11 Oktoba 2021 na Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu wakati akizungumza na waandishi wa habari, makao makuu ya chama hicho, Makumbusho mkoani Dar es Salaam.

“Muda aliyoomba Rais Samia kusimamisha nchi inatosha, miezi sita hii inatosha kabisa. Sasa Rais Samia aanzishe mchakato wa Katiba, tujadili na kutafakari wapi tunaanzia na tunaumaliza vipi kwani Katiba ni muhimu kwa mustakabali wa Taifa.”

“Lakini tumeshuhudia Rais Samia amekutana na makundi mbalimbali ya wanawake, wazee, vijana, asasi za kiraia na mengine, sasa Rais akutane na vyama vya siasa ili kujadili masuala ya siasa za Tanzania na kujenga mazingira ya kuheshimiana na siasa za kistaarabu,” amesema Ado

Tarehe 28 Julai 2021, Rais Samia akizungumza na waandishi na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, alisema anatambua umuhimu wa katiba lakini akaomba apewe muda ili aisimamishe nchi kiuchumi.

Katika mazungumzo yake leo, Ado amesema, kutokana na changamoto mbalimbali za chaguzi za marudio na chaguzi zote zilizopita kwa ujumla wake, Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe alimwandikia barua Rais Samia kumuomba kuchukua hatua ili chaguzi Tanzania ziwe huru, za haki na kuaminika.

Ado amesema, mageuzi ya msingi ambayo ACT Wazalendo wamedai wanayapigania kwenye mfumo wa uchaguzi na uendeshaji wa siasa kwa ujumla wake ni “kuanzishwa kwa mchakato wa kuzifanya Tume za Uchaguzi kufanya shughuli zake kwa uhuru.”

Rais Samia Suluhu Hassan

“Tunapendekeza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iwe na watumishi wake wanaowajibika kwa Tume tu na wasiwe ni makada wa chama kingine cha siasa. Hili tumeshuhudia hata tume yenyewe wakati inakabidhi ripoti kwa Rais ililisema hili,” amesema

“Kuanzishwa kwa mchakato shirikishi wa kupitia upya sheria ya vyama vya siasa ili kuondoa vifungu vyote vinavyobana uhuru wa vyama vya siasa kutekeleza majukumu yake. Vyama vya Siasa viwe na uhuru wa kufanya mikutano yake bila bugudha na hizi sheria si kuzibadili ni kuzifumua kabisa kabisa,” amesema

Ado amesema, kuanzishwa kwa majadiliano miongoni mwa vyama ili kujenga kuaminiana na kutatua migogoro kwa njia za amani pale inapotokea.

“Vyombo vya Ulinzi na Usalama vitende haki kwenye chaguzi na kuzifuta kesi zote zinazowakabili wanachama wetu na wa vyama vingine vya upinzani walizobambikiwa kwenye chaguzi,” amesema

1 Comment

  • Asante act vyema tuanze mchakato wa katiba mpya ndani ya chama chetu cha act maana ya kusema ivyo katiba ya chama chetu cha act imepitwa na wakati na inausulutani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!