Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Ugonjwa wa akili tishio
AfyaHabari Mchanganyiko

Ugonjwa wa akili tishio

Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Afya, anayeshughulikia magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Dk. James Kihologwe
Spread the love

 

TATIZO la afya ya akili duniani limeendelea kuwa tishio, huku ikikadiriwa kuwa litaongezeka kutoka asilimia 12 hadi 17 ifikapo mwaka 2030. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa jana tarehe 10 Oktoba 2021, jijini Dodoma na Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Afya, anayeshughulikia magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Dk. James Kihologwe, kwenye maadhimisho ya siku ya afya ya akili na kupinga matumizi ya pombe kupita kiasi duniani.

Dk. Kihologwe alisema tatizo la afya ya akili linachangiwa na sababu nyingi, ikiwemo unywaji pombe uliopitiliza, utumiaji wa dawa za kulevya, mawazo na sonona.

“Changamoto ya pombe na madhara yake ni makubwa, ambapo takwimu zinaonyesha tuna tatizo kubwa la vifo milioni tatu, vinavyotokana na pombe duniani. Huku wengine wakiwa na ulemavu wa maisha,” alisema Dk. Kihologwe.

Dk. Kihologwe alisema suala la afya ya akili ni mtambuka katika malezi na kwamba, kila mtu akitimiza majukumu yake kwa kukwepa visababishi vyake, tatizo hilo litapungua hadi kufikia asilimia moja.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Magonjwa yasiokuwa ya kuambukiza Wizara ya Afya, Dk.Shedrack Makubi, amesema takwimu zinaonyesha Tanzania kuna wagonjwa wa afya ya akili milioni saba, walioapata matibabu ni laki saba.

“Tunapaswa kuchukua hatua za haraka na kuwekeza zaidi katika magonjwa ya akili na afya ya akili, kwani tatizo hili limeonekana kukua siku hadi siku,” alisema Dk. Makubi.

Mbunge wa Viti Maalum mkoani Shinyanga, Salome Makamba ameitaka jamii kuachana na imani potofu dhidi ya tatizo la afya ya akili, bali wawapeleke wagonjwa kwenye Hospitali ya Mirembe mkoani Dodoma, badala ya kuwapeleka kwa Waganga wa kienyeji.

“Bado tunachangamoto kubwa katika jamii, ni ukweli usiopingika elimu juu ya magonjwa ya afya ya akili ni ndogo na wengi hudhani kwamba ukipata taitizo la akili, huwezi kupona jambo ambalo sio la kweli,” amesema Salome na kuongeza:

” Sasa hivi Serikali ipo kwenye mchakato kupitisha muswada, ili iwe sheria ya bima ya afya kwa kila Mtanzania. Lazima awe na bima ya afya na mimi kama mbunge mwakilishi wa wananchi napendekeza ugonjwa wa akili uingea kwenye matibabu ya bima ya afya.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!