Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko ACT-Wazalendo kuwasilisha kwa Rais Mwinyi maamuzi yake kuhusu SUK
Habari Mchanganyiko

ACT-Wazalendo kuwasilisha kwa Rais Mwinyi maamuzi yake kuhusu SUK

Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu
Spread the love

KAMATI Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo imeazimia kuwasilisha kwa Maakmu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Rais wa Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Nakala ya barua hiyo pia itawasilishwa kwa kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamebainishwa leo Jumapili tarehe 22 Januari, 2023 na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi jana makao makuu ya chama hicho.

Pia chama hicho kimeonesha nia ya kuonana na mabalozi wanaozikilisha nchi zao hapa nchini ili kuwaleza mwenendo usioridghisha wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

Shaibu amesema awali chama hicho kilipokea taarifa kutoka kwa wawakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa kuwa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa yamerejesha mahusiano mazuri na Zanzibar kutokana na uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

“Kamati Kuu imewaagiza viongozi wakuu wa Chama kuonana na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na serikali zao kuwaeleza mwenendo wa sasa usioridhisha wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar,” amesema Shaibu.

Mbali na kumwandikia barua pia chama hicho kimemtaka Rais Dk. Mwinyi kuweka wazi Ripoti ya Kikosi Kazi alichokiunda kushughulikia masuala ya demokrasia Zanzibar.

Shaibu amesema Dk. Mwinyi anapaswa kuiga mfano wa mwenzake Rais Samia Suluhu Hassan ambaye Ripoti ya Kikosi Kazi hake imewekwa wazi kwa umma na inapatikana kwenye tovuti.

“Penye nia ya dhati, masuala yanayogusa maslahi ya umma huwekwa wazi. Hakuna sababu inayohalalisha kufichwa kwa Ripoti ya Kikosi Kazi Zanzibar,” amesema Shaibu.

Shaibu ameongeza kuwa Kamati Kuu imeweka muda wa utekelezwaji wa makubaliano baina ya Rais Mwinyi na Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad waliyoyafanya kabla ya ACT Wazalendo kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Amezitaja hoja hizo kuwa ni kufanyika uchunguzi huru wa kimahakama kuhusu uvunjwaji wa haki za binadamu wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 na kuwapatia fidia wahanga wa uchaguzi huo na kufanyiwa mapitio na mabadiliko mfumo wa uchaguzi na Mahakama wa Zanzibar.

Amesema kuwa kwenye vikao mbalimbali Rais Mwinyi amekuwa akieleza kuwa hoja za maridhiano zitatekelezwa kwa ufanisi atakapochaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM.

“Tunataka utekelezaji kwa vitendo wa Hoja Tatu zilizowasilishwa kwa Rais Mwinyi,” amesisitiza Shaibu.

Amesema hadi sasa hoja iliyofanyiwa kazi ni ya kuachiwa huru viongozi wa ACT Wazalendo waliokuwa mahabusu au wameshikiliwa kwa njia nyingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!