Saturday , 18 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira
ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love

 

MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi ya uzalishaji wahitimu katika taaluma ambazo nafasi za ajira zimepungua ikiwemo walimu, badala yake ilekeze nguvu kwenye kuzalisha wahitimu wa mafunzo ya ufundi stadi, ambao ni rahisi kujiajiri. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Shangazi ametoa maoni hayo leo tarehe 22 Aprili 2024, bungeni jijini Dodoma, akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kwa mwaka wa fedha wa 2024/25, iliyowasilishwa na waziri wake, Prof. Kitila Mkumbo.

Mbunge huyo wa CCM amesema, sera ya elimu inapaswa kufanyiwa marekebisho ili iwe na mikakati ya kuzalisha watanzania ambao watakuja kuwa wazalishaji wazuri wa Taifa.

“Jambo mahususi nilitaka nishauri, bado tunazalisha sana watumishi katika kada ya walimu ambayo haiwezi kuajiri, vijana wengi wako mtaani hawajaajiriwa lakini bado vyuo vyetu vinaendelea kuzalisha walimu. Tunaomba wizara ilitizame hili jambo kwa upana kwamba kuna vyuo 35 vya Serikali vinazalisha walimu, je tuna umuhimu wa kuendelea kuwazalisha,” amesema Shangazi na kuongeza:

“Nadhani vizuri mipango ikatuelekeza tuwe na wanafunzi wengi kwenye vyuo vya aina ya DIT, huku tuwe na wanafunzi wengi ambao hata baadae hawatatusumbua kulazimika kuwatafutia ajira sababu watajiajiri wenyewe kulingana na maarifa watakayopata kupitia vyuo hivi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

Habari za SiasaTangulizi

Haya hapa majina walioteuliwa kugombea nafasi mbalimbali CHADEMA

Spread the loveCHAGUZI wa kanda za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Uingereza yamwaga bil. 9 kumuunga mkono Samia matumizi nishati

Spread the loveWaziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani...

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe abadili mbinu ya kudai Katiba mpya

Spread the loveMwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (Chadema), Fremaan Mbowe amebadili mbinu...

error: Content is protected !!