Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele
Habari Mchanganyiko

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Prof. Mkumbo
Spread the love

 

WIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake ya kiasi cha Sh. 121.3 bilioni, katika mwaka ujao wa fedha wa 2024/25. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa 2024/25, yamewasilishwa leo tarehe 22 Aprili 2024, bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo.

Prof. Mkumbo amesema Sh. 100.2 bilioni zimetengwa kutumika kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh. 21.8 zikipangwa kutumika katika miradi ya maendeleo.

Waziri huyo wa uwekezaji ametaja vipaumbele vitakayofanyiwa kazi 2024/25, ikiwemo ufufuaji mradi mkubwa wa eneo la kiuchumi la Bagamoyo, unaojumuisha ujenzi wa bandari mpya na ukanda maalum wa viwanda.

Prof. Mkumbo amesema katika mwaka ujao wa fedha wamepanga kutangaza mradi wa Bagamoyo kwa wawekezaji wa nje ya nchi, kwa nia ya kuendeleza mradi kwa njia mbalimbali, ikiwemo ubia na sekta binafsi kwa kufuata mpango uliorejewa.

“Tumepanga kufanya uendelezaji wa miradi ya kitaifa ya kielelezo, ikiwa nipamoja na kuanza hatua za awali za kuandaa mipango kabambe, upembuzi yakinifu, kufanya uthamini katika maeneo maalum ya uwekezaji ambayo hayakuthaminiwa awali na kufanya malipo ya fidia ya maeneo ya Bagamoyo, Tanga na Manyoni,” amesema Prof. Mkumbo.

Mkataba wa kuanza utekelezaji mradi huo ikiwemo ujenzi wa bandari ya kisasa ya Bagamoyo ulisainiwa Oktoba 2015 katika Serikali ya Awamu ya Nne, chini ya Rais mstaafu Jakata Kikwete, ambapo awamu ya kwanza ya utekelezaji wake ilitakiwa ikamilike 2017. Hata hivyo, mradi huo ulifutwa 2018 kwenye Serikali ya Hayati Dk. John Pombe Magufuli.

Mnamo Septemba 2023, Prof, Mkumbo alipokea taarifa ya upembuzi yakinifu na mpango wa ujenzi wa mradi huo, ambapo alisema utagharimu Sh. 11 trilioni ambapo utatumia hekta 9,800.

Mbali na ufufuaji mradi wa Bagamoyo, Prof. Mkumbo ametaja vipaumbele vingine vya wizara yake kwa 2924/25, ikiwemo kukamilisha uandaaji wa sera mpya ya uwekezaji na mkakati wake wa utekelezaji, kukamilisha uunganishaji wa kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)na mamlaka ya maeneo ya uzalishaji wa mauzo ya nje (EPZA).

Vingine ni kuanzisha taasisi mpya ya kusimamia masuala ya uwekezaji wa sekta binafsi, kukamilisha mwongozo wa ujenzi na uendeshaji wa kongani wa viwanda nchini.Kuendelea kusimamia utekelezaji wa mageuzi katika uendeshaji wa mashirika ya umma, ikiwemo kuendelea kubaini mashirika ambayo majukumu yake yamepitwa na wakati au yanaingiliana na majukumu ya taasisi zingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!