Wednesday , 22 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yatoa ajira watumishi 46,000, yatangaza utaratibu mpya kuajiri
Habari Mchanganyiko

Serikali yatoa ajira watumishi 46,000, yatangaza utaratibu mpya kuajiri

Spread the love

SERIKALI imetangaza nafasi za ajira za watumishi wa umma 46,000 katika sekta mbalimbali, ikiwemo  12,000 katika sekta ya elimu na zaidi ya 10,000 kwenye sekta ya afya. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es salaam…(endelea).

Akizungumza bungeni jijini Dodoma, leo tarehe 17 Aprili 2024, Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene,amesema jana Jumanne, Rais Samia Suluhu Hassan, ametoa kibali cha nafasi hizo za ajira.

Simbachawene amesema katika ajira za walimu wataajiri kwa utaratibu wa kutafuta watumishi kutoka kwenye maeneo yenye upungufu wa wailimu.

“Rais siku ya jana ametoa kibali cha kaujiri watumishi wapya 46,000 na katika idadi hiyo kibali cha ajira za walimu ni 12,000 na afya zaidi ya 10,000. Kwa hiyo imani yangu kwamba kwa kushirikiana na serikali tutahakikisha upungu wa walimu unaondoka na penye upungufu mkubwa tunafikiri kuwa na utaratibu mpya wa kuajiri kupitia kwenye mikoa badala ya central,” amesema Simbachawene.

Kufuatia kauli hiyo, Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu, ameitaka Serikali kuwapata kipaumbele cha ajira kwa walimu waliojitolea kwa zaidi ya miaka mitatu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hukumu mahakama kuu yabatilishwa kesi State Oil, Equity Bank Tz

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imebatilisha hukumu iliyotolewa...

Habari Mchanganyiko

Geita, Mwanza waongoza kwa mbwa

Spread the loveNaibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema taarifa...

Habari Mchanganyiko

Waziri aipongeza NBS kwa mafanikio

Spread the love  Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande amepongeza Ofisi ya...

Habari Mchanganyiko

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk....

error: Content is protected !!