Tuesday , 21 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Faye amteua aliyekuwa mfungwa mwenzie kuwa waziri mkuu
Habari za SiasaKimataifa

Rais Faye amteua aliyekuwa mfungwa mwenzie kuwa waziri mkuu

Spread the love

Rais mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amemteua Ousmane Sonko kama Waziri Mkuu saa chache baada ya kuapishwa kuwa mkuu wa nchi hiyo jana Jumanne. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Taarifa ya uteuzi huo ilisomwa jana jioni na Katibu Mkuu wa ofisi ya rais Senegal, Oumar Samba Bâ katika kituo cha televisheni ya taifa – RTS.

“Ninapima umuhimu wa imani ambayo Rais Faye ameniwekea,” amesema Ousmane Sonko kwenye RTS, wakati akimshukuru Faye na kumhakikishia uaminifu na kumuahidi kujitolea kwake katika ujenzi wa taifa hilo.

Sonko ambaye ni Mwanzilishi huyo wa chama cha PASTEF, licha ya kwamba hakuweza kuwa mgombea wa urais, ameweka historia ya kipekee kutokana na safari ya kisiasa ya wawili hao.

“Wakati wa mkutano ambao ulifunga kampeni zetu za uchaguzi, nilisema kwamba sote tunafanya kazi ya kumchagua Rais Bassirou Diomaye Faye. Hakutakuwa na suala la kumwacha peke yake kuchukua jukumu hili.

“Ningependa kuwaambia Wasenegali, kwa kila mmoja, popote pale alipo, kwamba jukumu hili ni lao. Kila mtu atalazimika kujitolea vilivyo zaidi ili tufikie malengo ambayo tumeweka kwa Senegal na sio kwa rais,” alisema Sonko.

Alisema serikali wanayoenda kuiunda watajitolea kwa hali na mali kuhakikisha wanayafikia malengo waliyowaahidi Wasenegali ambayo ni kuwakwamua katika mdororo wa uchumi,kuwaletea maendeleo na kuwa mfano wa mabadiliko ya kweli na sahihi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the loveKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akwaa kisiki, mahakama yamzuia kuwani urais

Spread the loveMahakama ya katiba nchini Afrika Kusini, katika uamuzi wake imesema...

Habari za SiasaKimataifa

Kiongozi Mkuu Iran amteua mrithi wa Rais Ebrahim

Spread the loveKiongozi wa ngazi ya juu nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei,...

error: Content is protected !!