Monday , 20 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa DRC wampata waziri mkuu wa kwanza mwanamke
Kimataifa

DRC wampata waziri mkuu wa kwanza mwanamke

Judith Suminwa
Spread the love

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi amemteua waziri wa mipango, Judith Suminwa kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Suminwa ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo wa waziri mkuu nchini Kongo. Uteuzi wa Suminwa unakamilisha wiki kadhaa zilizoghubikwa na hali ya sintofahamu kuhusu wadhifa huo.

Katika hotuba kupitia televisheni ya taifa, Suminwa amesema kuwa anafahamu kuhusu jukumu kubwa linalomkabili ni kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuhakikisha kuwepo kwa amani na maendeleo nchini humo.

Kuapishwa kwa Tshisekedi kwa muhula wa pili madarakani mwezi Januari, kulianzisha mchakato wa muda mrefu wa kutafuta muungano wa vyama vingi katika bunge la kitaifa, ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuteuliwa kwa waziri mkuu na kuundwa kwa serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Rais Iran afariki kwa ajali ya helkopta

Spread the loveRais wa Iran, Ebrahim Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje...

Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Spread the loveAliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter...

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

error: Content is protected !!