Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mkeka wa Samia: Ndalichako, Makala nje, Migiro, Ndejembi waula
Habari za SiasaTangulizi

Mkeka wa Samia: Ndalichako, Makala nje, Migiro, Ndejembi waula

Spread the love

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali wakiwamo wakuu wa wilaya, mikoa, mawaziri na manaibu mawaziri. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Miongoni mwa waliotenguliwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako ambaye nafasi yake imechukuliwa na Deogratius John Ndejembi.

Kabla ya uteuzi huu Ndejembi alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Katika taarifa iliyotolewq leo Jumamosi na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikuli, Zuhura Yunus imesema pia Samia a memteua Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Kabla ya uteuzi huu Makonda alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Amos Makala

Anachukua nafasi ya John Vianney Mongella ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Rais Samia pia amemteua Kanali Evans Alfred Mtambi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara. Kabla ya uteuzi huu Kanali Mtambi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.

Amemhamisha Said Mohamed Mtanda kutoka Mkoa wa Mara kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Mtanda anachukua nafasi ya Amos Gabriel Makalla ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Amemteua Zainab Athuman Katimba (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Zainab anachukua nafasi ya Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ambaye ameteuliwa kuwa Waziri.

Amemteua Daniel Baran Sillo kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Sillo anachukua nafasi ya Mhe. Jumanne Abdallah Sagini ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria.

Amemhamisha Mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi kutoka Wizara ya Maji kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Deogratius Ndechembi

Amemhamisha Kundo Andrea Mathew kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji.

Amemteua Fakii Raphael Lulandala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro. Kabla ya uteuzi huu Lulandala alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM).

Amemteua Gilbert Kalima kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga. Kabla ya uteuzi huu Bw. Kalima alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi.

Amemhamisha Mhandisi Cyprian John Luhemeja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Amemhamisha Mary Ngelela Maganga kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

Amemteua Dk. Edwin Paul Mhede kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Dk. Mhede aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).

Dk. Mhede anachukua nafasi ya Agnes Kisaka Meena ambaye amehamishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji.

Amemteua Dk. Suleiman Hassan Serera kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huu Dk. Serera alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.

Dk. Serera anachukua nafasi ya Nicholaus Mkapa ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia wa Habari.

Amemteua Selestine Gervas Kakele kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Kakele alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Amemteua Balozi Dk. Asha Rose Migiro kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango.

Uapisho wa Waziri, Wakuu wa Mikoa, Naibu Mawaziri na Naibu Makatibu Wakuuu tafanyika tarehe 04 Aprili, 2024 saa 05:00 asubuhi Ikulu, Dar es Salaam.

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yatoa kauli wanaolala nje Hospitali ya Muhimbili

Spread the loveSERIKALI imesema inajipanga kushirikiana na sekta binafsi kujenga majengo yatakayosaidia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara yaomba bajeti ya Sh. 67.9 bilioni, wamachinga watengewa bilioni 10

Spread the loveBAJETI ya Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Migogoro ya ndoa yaongezeka, Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveMIGOGORO ya ndoa na familia imeongezeka kwa asilimia 8.3  kutoka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yahamasisha uanzishaji vituo vya kulea watoto wachanga

Spread the loveSERIKALI imewahimiza wananchi kujenga vituo vya kulelea watoto wadogo na...

error: Content is protected !!