Sunday , 12 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Museveni amteua mwanaye kuwa mkuu wa majeshi
Habari MchanganyikoKimataifa

Rais Museveni amteua mwanaye kuwa mkuu wa majeshi

Spread the love

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amemteua mtoto wake wa kiume Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa mkuu wa majeshiya nchi hiyo uteuzi ambao umetajwa kudhihirisha wazi kuwa huenda kiongozi huyo anamuandaa mtoto wake kumrithi atakapoachia madaraka. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Muhoozi Kainerugaba anachukua nafasi ya Jenerali Wilson Mbasu Mbadi ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa biashara katika mabadiliko mapya ya baraza la mawaziri yaliyotangazwa jana jioni.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi, washauri wake wawili wa karibu pia wamepewa nyadhifa za uwaziri na kuchochea uvumi kwamba Rais Museveni anaunga mkono shughuli za kisiasa Muhoozi Kainerugaba.

Mtoto huyo wa kwanza wa rais amekuwa akifanya mikutano ya hadhara kote nchini, hatua ambayo inakwenda kinyume na sheria inayowazuia maafisa wa jeshi kujihusisha na siasa.

Kainerugaba hata hivyo amejitetea kwa kueleza kuwa shughuli zake – ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa hivi karibuni wa kundi la uanaharakati la Patriotic League of Uganda – aliyesema kundi hilo linanuia kuhimiza kujenga uzalendo miongoni mwa Waganda.

Museveni ambaye kwa mara ya kwanza alichukua madaraka kwa nguvu mnamo mwaka 1986, na kuchaguliwa mara sita, hajaeleza ni lini atakapostaafu.

Kiongozi huyo pia hana mpinzani ndani ya chama tawala cha NRM huku wengi wakiamini kuwa jeshi litakuwa na sauti katika kuchagua mrithi wake.

Kulingana na wachambuzi, washirika wa Kainerugaba wameteuliwa kimkakati kwenye nafasi za juu za idara ya usalama. Uganda itaanda uchaguzi mkuu ujao mwaka 2026.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

error: Content is protected !!