Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Shule zafungwa kutokana na ongezeko la joto
Habari MchanganyikoKimataifa

Shule zafungwa kutokana na ongezeko la joto

Spread the love

SUDAN Kusini imeamuru kufungwa kwa shule zote kuanzia leo Jumatatu, ikiwa ni hatua ya tahadhari kutokana na joto kali linalotarajiwa kudumu kwa wiki mbili. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Wizara za afya na elimu zimetoa ushauri kwa wazazi kuwabakisha watoto wao nyumbani, kwa sababu viwango vya joto vinatarajiwa kufikia nyuzi 45.

Serikali imesema shule yoyote itakayokiuka agizo hilo na kuendelea kufungua wakati wa kipindi cha tahadhari itafutiwa usajili wake.

Hata hivyo, tahadhari hiyo iliyotolewa usiku wa kuamkia Jumapili haikufafanua ni kwa muda gani shule zitafungwa.

Sudan Kusini, taifa changa zaidi barani Afrika linakabiliwa na hatari ya athari ya mabadiliko ya tabia nchi na joto kali. Lakini ni nadra sana kwa viwango vya joto nchini humo kupita nyuzi 40 katika vipimo vya Celsius.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DAWASA yatekeleza agizo la Samia kwa kutangaza zabuni kielektroniki

Spread the loveKiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Godfrey Mnzava...

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

error: Content is protected !!