Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wavuvi 9 wanusurika kifo boti ikizama Coco Beach
Habari Mchanganyiko

Wavuvi 9 wanusurika kifo boti ikizama Coco Beach

Spread the love

WATU tisa wamenusurika kufa baada ya boti ya uvuvi ya My Legacy inayomilikiwa na Yakoub Juma, kuzama katika baharini maeneo ya ufukwe wa Coco Beach, jioni ya tarehe 10 Machi 2024. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 11 Machi 2024 na Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), walionusurika kifo ni wavuvi sita, mhandisi wa mitambo mmoja na manahodha wawili.

Taarifa hiyo imesema kuwa, Kituo  cha kuratibu shughuli za utafutaji na uokoaji cha TASAC (MRCC) kilipokea taarifa ya kuzama kwa boti hiyo kisha kuanza zoezi la ukokoaji lililofanikisha kuokoa maisha wa watu hao.

“MRCC kilifanya jukumu lake la kisheria la kuratibu shughuli ya uokoaji kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi (Wanamaji) na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na kufanya juhudi za kufika eneo la tukio na kufanya zoezi la uokoaji. Watu wote tisa wamefanikiwa kuokolewa na wanaendelea vizuri kiafya bila ya kuwa na changamoto yoyote,” imesema taarifa hiyo.

Chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa, boti ilikuwa kwenye majaribio ya kiufundi baada ya matengenezo ya mifumo ya uvuaji samaki kwa kukokota, ambapo ilianzia maeneo ya Tandavamba Kivukoni na kuzunguka kwenye maeneo yenye maji mafupi karibu na eneo la daraja jipya la Tanzania (Upanga) hadi Coco Beach (Oysterbay).

“Ilipofika majira ya saa 9:50 Alasiri wakati nahodha anabadilisha uelekeo wa boti kuelekea upande wa kulia ndipo kamba moja ya upande wa kushoto ikakatika na kusababisha uzito kelemea kwenye kamba ya upande wa kulia na ndipo uzito ulipohama ghafla na kuilazimisha boti kunywa maji upande wa kulia kisha kuzama,” imesema taarifa hiyo na kuongeza:

“TASAC inaendelea kutoa rai kwa wamiliki na waendeshaji wa vyombo majini kuzingatia Sheria na Kanuni za udhibiti usafii majini na kuhakikisha muda wote wanavalia majaketi okozi ili kujiepusha na maafa yanayoweza kusababishwa na tukio la ajali.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile aukwaa uenyekiti wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!