Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Benki ya Dunia yatoa somo kwa Regrow
Habari Mchanganyiko

Benki ya Dunia yatoa somo kwa Regrow

Spread the love

 

WATAALAM kutoka Benki ya Dunia wanaendesha semina kwa Wataalam wanao simamia utekelezaji wa Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) juu ya mfumo wa upokeaji na kushughulikia malalamiko pale yanapotokea wakati wa utekelezaji wa mradi. Anaripoti Yusuph Kayanda, Morogoro … (endelea).

Akifungua Mafunzo hayo Mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa Kitengo cha Utafiti na Mafunzo, Dk. Edward Kohi ameipongeza Benki ya Dunia kwa kuandaa Mafunzo hayo ambayo yataimarisha zoezi zima la upokeaji wa malalamiko na namna ya kuyashughulikia kwa wakati ili malengo ya mradi yafikiwe kwa wakati.

Dk. Kohi ameongeza kuwa mfumo huo wa REGROW wa kupokea malalamiko ni muhimu kwakuwa unatoa nafasi kwa wananchi na wadau mbalimbali kutoa malalamiko au maoni yenye nia ya kuboresha zoezi zima la utekelezaji wa mradi kwa njia shirikishi.

Aidha ametoa wito kwa washiriki kuzingatia Mafunzo hayo ili kupata uelewa mpana wa kughulikia malalamiko si kwa mradi tu wa REGROW bali kwenye kazi za kilasiku za Wizara ya Maliasili na Utalii.

Wakizungumzia mafunzo hayo ya siku mbili, Maafisa Wandamizi wa Maendeleo ya Jamii Benki ya Dunia, Roselyn Kaihula na Bi. Annette Omolo, wamesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wataalam wanotekelezaji mradi wa REGROW, namna ya kushughulikia malalamiko na changamoto mbalimbali kwa ufanisi zaidi hali itakayo pelekea zaidi kufikiwa kwa malengo kusudiwa ya mdari huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!