Monday , 13 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mgomo kitita kipya cha NHIF: Serikali yaita hopsitali binafsi mezani
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mgomo kitita kipya cha NHIF: Serikali yaita hopsitali binafsi mezani

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
Spread the love

SERIKALI imekiita mezani Chama cha Wenye Hospitali Binafsi (APHFTA), ili kutafuta suluhu ya mvutano wao kuhusu matumizi ya kitita kipya cha gharama za matibabu,  cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 1 Machi 2024 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akizungumza na waandishi wa habari,  baada ya APHFTA kutangaza kugomea kitita hicho kwa madai kuwa kitaua biashara zao kwa kuwa hospitali zitashindwa kujiendesha kutokana na ongezeko la gharama za maisha, huku gharama za matibabu zikishushwa.

“Leo watuambie kama vigezo vilivyowekwa na kamati hawakubaliani navyo kwa sababu hakuna vigezo vingine. Gharama za dawa wametumia kiasi gani, gharama za uendeshaji na faida waje mezani waseme mmetuwekea faida ndogo. Waje mezani waseme dawa hii haiuzwi bei hii ndio ushahidi tunao sio kusema hatutaki kitita, leteni hoja zenu,” amesema Ummy.

Ummy amesema APHFTA wanapaswa kuweka mezani vigezo vyao ili vilinganishwe na vigezo vya kitita cha NHIF, ili kuangalia namna ya kupata vigezo vitakavyoafikiwa na pande zote mbili katika ukokotoaji wa gharama au bei za huduma za afya.

Katika hatua nyingine, Ummy amesema kitita hicho kimeanzishwa baada ya wizara yake pamoja na wadau wa sekta ya afya kuketi mezani na kutoa mapendekezo juu ya namna ya kukiandaa.

“Tulifanya kikao cha pamoja na wadau wa NHIF ikiwemo wamiliki wa hospitali binafsi, tume ya kikristo ya huduma za jamii, kamati ya afya chini ya BAKWATA na wenine, wakakutana wakasikiliza hoja za NHIF, wakasikiliza hoja za hospitali binafsi, kamati ikaja na vigezo kuhusu maboreshi ya kitita ambcho NHIF imeleta na wao walileta bila kuathiri upande wowote,” amesema Ummy.

Msimamo huo wa Serikali, umekuja baada ya APHFTA kutangaza kuanza mgomo wa kutohudumia wateja kupitia kitita hicho kipya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

error: Content is protected !!