Sunday , 12 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Asiyeamini sanamu ya Nyerere amuulize Madaraka’
Habari za SiasaTangulizi

‘Asiyeamini sanamu ya Nyerere amuulize Madaraka’

Spread the love

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Mussa Shaib amesema sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere iliyotengenezwa na kuzinduliwa katika Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa nchini Ethiopia, imetengenezwa kwa uhalisia asilimia 92 na ambaye haamini kuwa siye baba wa Taifa akamuulize mwanaye Madaraka Nyerere. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

“Msihusishe sanamu ya Mwalimu Nyerere na uhalisi wake wa miaka ya 1990 kuendelea, sanamu ile imetengenezwa kwa uhalisia wakr wa miaka 1960- 1980,’ amesema.

Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu huyo amesema sanamu hiyo ilipotolewa kwenye tanuru nchini Ubelgiji iliidhinishwa na kamati ya wataalamu mbalimbali akiwamo mtoto wa Mwalimu Nyerere.

Ametaja kamati hiyo kuwa iliundwa na wabobezi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wizara ya sanaa, utamaduni na michezo, wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa pamoja mtoto wa baba w Taifa, Madaraka Nyerere.

“Madaraka mwenyewe amewaeleza waandishi wa habari kama kuna mtu ambaye haamini yule ni Mwalimu Nyerere basi aende amuulize yeye, au nendeni mkamuulize Dk. Damas Ndumbaro,”  amesema Balozi Shaibu.

1 Comment

  • Duh! Miaka ile Nyerere alikuwa na mashavu ya mviringo. Huyo wamemkondesha bure. Swali kwa hao wataalamu na Madaraka.
    Mlishindanisha wasanii?
    Modeli iliyoshinda tuonyesheni!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!