Wednesday , 15 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia: Lowassa hakukubali kuyumbishwa
Habari za Siasa

Rais Samia: Lowassa hakukubali kuyumbishwa

Kaburi la Hayati Edward Lowassa
Spread the love

 

ALIYEKUWA Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Hayati Edward Lowassa, hakukubali kuyumbishwa katika utekelezaji wa majukumu yake serikalini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamelezwa leo tarehe 17 Februari 2024 na Rais Samia Suluhu Hassan, akitoa salamu zake katika mazishi ya mwili wa Lowassa, yaliyofanyika Monduli, mkoani Arusha.

Rais Samia amesema Lowassa atakumbukwa kwa usimamizi na ufuatiliaji wake aliposhika nyadhifa mbalimbali serikalini, pamoja na kujitoa mhanga. Amesema atakumbukwa kwa ubunifu wake katika uundwaji wa mamlaka za maji za miji mikuu ya mikoa uliosaidia upatikanaji maji safi kwa wananchi na huduma ya uondoaji maji taka.

“Somo hapa ni kwamba ukipewa dhamana za uongozi kwa kuaminiwa katika nafasi mbalimbali lazima tuwe na uthubutu na ubunifu na kujitoa mhanga kusimamia na kutekeleza maelekezo ya serikali kwa weledi na uaminifu bila kukubali kuyumbishwa,” amesema Rais Samia.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amesema Lowassa alikuwa mpenzi wa demokrasia, uhuru wa mawazo na uchambuzi wake. Amesema ameacha mafunzo makubwa matatu ambayo ni ustahimilivu, ushupavu na ulezi.

“Ndugu yetu alikuwa kiongozi jasiri na shupavu, alionyesha ushupavu nyakati mbalimbali wakati wa uongozi wake, alipokuwa waziri wa maji licha ya shinikizo kubwa la kutotumia maji ya Ziwa Victoria kwa sababu za kihistoria, kwa ujasiri na ushupavu mkubwa wa uongozi aliishauri vyema serikali na kuweka msukumo hadi maji yanatumika katika mikoa ya Shinyanga na Tabora na tumeshaamua mradi huo ufike Singida na Dodoma,” amesema Rais Samia.

Amesema kifo cha Lowassa kilichotokea tarehe 10 Februari mwaka huu, akipatiwa matibabu kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam, kimeacha pigo kwa familia na taifa.Amesema Serikali na familia zilijitahidi kuhakikisha afya yake inaimarika lakini kudra ya Mungu imechukua nafasi yake.

Lowassa alizaliwa tarehe 26 Agosti 1953, katika uongozi wa kisiasa aliwahi kushika nyashifa mbalimbali serikalini, ikiwemo uwaziri mkuu na uwaziri wa maji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Madeleka aibwaga Jamhuri kesi za kubambikiwa

Spread the loveWakili Peter Madeleka ameshinda rufaa yake namba 263 ya mwaka...

Habari za SiasaTangulizi

Sheikh Ponda ataka kura ya maoni kuamua hatma ya muungano

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

Habari za Siasa

Bunge lakemea utoroshwaji mifugo kuelekea Kenya

Spread the loveKamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na...

Habari za Siasa

CUF yajipanga kuelekea chaguzi zijazo

Spread the loveCHAMA cha Wananchi (CUF), kimejipanga kujijenga kisiasa kuelekea chaguzi zijazo...

error: Content is protected !!