Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi yaruhusu maandamano ya Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Polisi yaruhusu maandamano ya Chadema

Spread the love

MAANDAMANO yasiyo na kikomo yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa ajili ya kupinga miswada ya marekebisho ya sheria za uchaguzi iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma, pamoja na kudai katiba mpya, yameruhusiwa na Jeshi la Polisi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, leo Jumatatu, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, amesema ruhusa ya maandamano hayo yaliyopangwa kuanza tarehe 24 Januari mwaka huu, imetolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Jumanne Muliro. baada ya viongozi wa chama chake kuzungumza naye.

Maandamano Chadema

“Team yetu ya chama ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Bara, Benson Kigaila imekuwa na kikao na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Dar Es Salaam ACP Jumanne Muliro na timu yake kuhusiana na maandamano ya amani yanayopangwa na kuratibiwa na Chadema siku ya Jumatano, 24 Januari 2024,” ameandika Mbowe na kuongeza:

“Makubaliano yamefikiwa kuwa maandamano yaendelee kama yalivyopangwa. Nalipongeza Jeshi la Polisi kwa busara hii. Karibuni Watanzania wote, tuandamane kwa Amani. “

Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam

Chadema kiliitisha maandamano hayo yasiyo na kikomo hadi Serikali itapoondoa bungeni miswada hiyo iliyowasilishwa Novemba 2023, kwa ajili ya kuifanyia marekebisho kwa kujumuisha maoni na mapendekezo ya wadau yaliyoachwa, hususan la upatikanaji wa tume huru ya uchaguzi pamoja na maamuzi ya tume ya taifa ya uchaguzi kuhojiwa mahakamani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!