Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu: Nitakuwepo Dar kushiriki maandamano ya amani
Habari za SiasaTangulizi

Lissu: Nitakuwepo Dar kushiriki maandamano ya amani

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) – Bara, Tundu Lissu ametangaza kushiriki maandamano ya amani yaliyoitishwa hivi karibuni na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mbowe alitangaza maandamano hayo yatakayofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 24 Januari mwaka huu kuishinikiza Serikali kuzingatia maoni na mapendekezo ya wadau wa uchaguzi nchini.

Akizungumza na Watanzania kwa njia ya mtandao leo Jumamosi kutokea jijini Abidjan nchini Ivory Coast kunakofanyika fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON), Lissu alisema mbali na kuwepo jijini humo kuiunga mkono Timu ya Taifa (Taifa Star) masuala ya siasa ya Tanzania ni muhimu.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

“Mimi nitakuwepo Dar es Salaam nitashiriki maandamano ya amani ya siku ya tarehe 24 ya wiki ijayo lakini hili haliwezi kuwa jukumu langu au la Mbowe peke yake au Chaderma peke yao kwa sababu katiba bora mpya na mfumo bora wa uchaguzi vinatuhusu sisi wote.

“Hivyo naomba kila mmoja wetu ajitafakari na atafakari katika mapambano haya na katika ustawi wa Taifa letu… natoa rai kwa wananchi wa Tanzania na wenye nia njema na nchi yetu nao wawepo Dar es Salaam siku hiyo ya kihistoria ili nao washiriki katika maandamano haya ya amani,” amesema Lissu.

Lissu amesema katika wa miswada mitatu iliyopelekwa bungeni Novemba mwaka jana ni wazi CCM haitaki kufanya mabadiliko yoyote ya maana kwa mfumo wa katiba na uchaguzi.

“Hata baada ya mazungumzo ya mwaka jana, Rais Samia Suluhu Hassan licha ya ahadi zake nyingi ndani na nje ya Tanzania, amekataa maridhiano ya kisiasa ambayo yangeondoa nchi kwenye kivuli cha utawala wa kiimla wa chama kimoja na madhara yake yote kwa nchi yetu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yatoa kauli wanaolala nje Hospitali ya Muhimbili

Spread the loveSERIKALI imesema inajipanga kushirikiana na sekta binafsi kujenga majengo yatakayosaidia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara yaomba bajeti ya Sh. 67.9 bilioni, wamachinga watengewa bilioni 10

Spread the loveBAJETI ya Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Migogoro ya ndoa yaongezeka, Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveMIGOGORO ya ndoa na familia imeongezeka kwa asilimia 8.3  kutoka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yahamasisha uanzishaji vituo vya kulea watoto wachanga

Spread the loveSERIKALI imewahimiza wananchi kujenga vituo vya kulelea watoto wadogo na...

error: Content is protected !!