Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia awataka wakulima wa karafuu kuacha biashara za magendo
Habari za Siasa

Rais Samia awataka wakulima wa karafuu kuacha biashara za magendo

Spread the love

WAKULIMA wa karafuu visiwani Zanzibar, wametakiwa kuacha kuuza kwa magendo zao hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus, wito huo ameutoa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 9 Januari 2024, alipozindua jengo la Kitega Uchumi la Zanzibar State Trade Cooperation (ZSTC), lililopo Chakechake kisiwani humo.

Rais Samia aliahidi kwamba serikali italeta wawekezaji wa karafuu ili kuimarisha mnyororo wa thamani wa zao hilo katika soko la dunia.

“Rais Samia amewataka wakulima wa karafuu kuacha kuchepusha na kuuza kwa magendo zao la karafuu. Pia, amewataka wakulima kuendelea kulima karafuu kwa wingi na kwa tija zaidi ili kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo na kuinua uchumi wa buluu,” imesema taarifa ya Yunus na kuongeza:

“Vilevile Rais Samia amesema serikali itaendelea kutafuta fursa za kuongeza tija na uzalishaji bila kuathiri viwango na thamani ya karafuu katika soko la kimataifa. Kwa upande mwingine ametoa wito wa ZSTC kutatua kero za wakulima pamoja na kuwa na kanzidata ili kutunza kumbukumbu za zao hilo na wakulima zitakazowezesha kuratibu mipango endelevu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RUWASA yachongewa, yateketeza mamilioni kwa maji yenye magadi

Spread the loveSAKATA la ukosefu wa maji wilayani Momba mkoani Songwe limezidi...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

error: Content is protected !!