Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Serikali yasitisha bei mpya kitita cha NHIF
AfyaTangulizi

Serikali yasitisha bei mpya kitita cha NHIF

Spread the love

Serikali ya Tanzania imesitisha bei mpya za kitita cha matibabu kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambazo zilipangwa kutekelezwa kuanzia tarehe 1 Januari 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Pia imetangaza kuunda kamati huru itakayofanya maboresho ya mapitio ya kitita cha mafao kwa mwaka 2023 yaliyofanyika ambayo awali yalifanywa na NHIF tarehe 18 Disemba mwaka jana na kuja na bei mpya zilizopangwa kuanza kutumika kuanzia mwezi huu.

Hatua hiyo imekuja baada ya hospitali binafsi kutishia kusitisha huduma za matibabu kwa wenye kadi za NHIF na kumlazimu Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kukutaza kwa mazungumzo na wadau hao ili kufikia muafaka.

Waziri Ummy amekutana na wawakilishi wa wamiliki wa hospitali binafsi wakiwamo Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC), Chama cha Wamiliki wa Vituo vya Aafya Binafsi Tanzania (APHFTA) na Bakwata jana tarehe 4 Januari 2023 jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, Waziri Ummy amewataka wawakikishi hao kujadiliana na kutoa maoni yao kwa uwazi na kwa kutanguliza maslahi mapana ya Watanzania ili kuwezesha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wananchi bila kikwazo cha fedha.

Katika mabadiliko ya ada ya usajili na ushauri wa daktari, viwango ambavyo vilipunguzwa ni kwa mgonjwa kumuona daktari Hospitali ya Taifa kufikia Sh25,000 kutoka Sh35,000 kwa daktari bingwa mbobezi na Sh20,000 kutoka Sh 25,000 kwa daktari bingwa.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

Mabadiliko mengine ni kwenye Hospitali ya Rufaa ya kanda na kumuona daktari bingwa mbobezi ni Sh25,000 kutoka Sh35,000  na kumuona daktari bingwa ni Sh20,000 kutoka Sh25,000.

Hospitali ya mkoa, kumuona daktari bingwa mbobezi ni Sh25,000 kutoka Sh Sh15,000 na kwa daktari bingwa ni Sh20,000 kutoka Sh15,000.

Pia, kwa kliniki bobezi, kumuona daktari bingwa mbobezi na daktari bingwa ni Sh10,000 kutoka Sh15,000 na kwenye kliniki nako kumuona daktari bingwa na bingwa mbobezi  ni Sh10,000.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Hatuoni faida ya demokrasia

Spread the loveMwenyekiti wa Chadema, Fremaan Mbowe amesema Tanzania haijanufaika na miaka...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ataka wananchi wasiruhusu bakora za Magufuli

Spread the loveMwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Profesa Ibrahimu Lipumba...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mbunge Mwakasaka alitaka Jeshi la Polisi kutenda haki

Spread the loveEMMANUEL Adamson Mwakasaka, Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), amelitaka Jeshi...

Habari za SiasaTangulizi

Madeleka aibwaga Jamhuri kesi za kubambikiwa

Spread the loveWakili Peter Madeleka ameshinda rufaa yake namba 263 ya mwaka...

error: Content is protected !!