Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kigogo CCM: Hatuwezi kushinda uchaguzi kwa mabavu
Habari za Siasa

Kigogo CCM: Hatuwezi kushinda uchaguzi kwa mabavu

Issa Gavu
Spread the love

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Idara ya Oganaizesheni, Issa Gavu, amesema chama hicho hakiwezi kushinda kwa kutumia njia za mabavu katika chaguzi, bali ili kishinde kinatakiwa kuandaa wagombea bora pamoja na kuhamasisha wananchi washiriki zoezi hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga…(endelea).

Gavu ametoa kauli hiyo jana Jumanne, akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM mkoani Shinyanga.

Katibu huyo wa organaizesheni CCM, alisema chama hicho kinapaswa kuandaa utaratibu wa kuwa na viongozi wawajibikaji, wanaojituma na kufanya kazi, ili waweze kuaminiwa na wananchi.

“Tunakwenda mwaka kesho utakuwa mwaka wa uchaguzi, njia pekee ya kuhakikisha kwamba chama chetu kinashinda ni kutengeneza utaratibu mzuri wa kuwa na viongozi wawajibikaji, wanaoweza kujituma na kufanya kazi. Hatuwezi kushinda kwenye mfumo wa vyama vingi kwa kutumia njia za mabavu,” alisema Gavu na kuongeza:

“Ili muende vizuri utakapofika wakati wa uboreshaji daftari la wapiga kura tuhakikishe tunahamasisha wanachama na wananchi wetu wajitokeze kwa wingi wakajiandikishe katia daftari ili ukifika wakati chama chetu kiwe na watu wengi waliojiandikisha ili mwisho wa siku kura zetu ziwe nyingi kuliko vyama vingine.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!