Saturday , 11 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa DPP afuta kesi ya Gekul, Madeleka kukata rufaa
Habari za SiasaTangulizi

DPP afuta kesi ya Gekul, Madeleka kukata rufaa

Spread the love

OFISI ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), imeondoa mahakamani kesi ya jinai Na. 179/2023, iliyofunguliwa na Hashim Ally dhidi ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Pauline Gekul. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hati ya kuiondoa mahakamani kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na Ofisi ya DDP Mkoa wa Manyara. Kesi hiyo ya jinai ilitarajiwa kuanza kusikilizwa leo tarehe 27 Disemba 2023, mahakamani hapo.

Wakili Madeleka

Barua hiyo ya ofisi ya DDP Manyara kwenda Mahakama ya Wilaya ya Babati imesema “mahakama imearifiwa na DPP kwa niaba ya jamhuri kuwa haitaki tena kumfungulia mashtaka Gekul kwa kosa la shambulio la kudhuru mwili kinyume na kifungu cha 241 cha kanuni ya adhabu ambayo ameshtakiwa nayo mbele ya mahakama tukufu.”

Kufuatia uamuzi huo, wakili wa Ally, Peter Madelekea, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X zamani kama Twitter, amesema wamekata rufaa katika Mahakama Kuu, kupinga uamuzi wa DPP kuifuta kesi hiyo akidai ni kinyume cha sheria kwa kuwa hakuifungua yeye.

“DPP ameiondoa mahakamani kinyume cha sheria kesi iliyokuwa inamkabili Pauline Philipo Gekul. Tumekata rufaa. Mahakama ya Wilaya ya Babati leo tarehe 27 Disemba 2023 imepokea kusudio la kukata rufaa kati ya Hashimu Ally dhidi ya Gekul,” ameandika Wakili Madeleka.

Ally anamshtaki  Gekul  akimtuhumu kwa kumfanyia shambulio lililosababisha madhara ya mwili, kinyume na kifungu cha 241 cha kanuni ya adhabu sura ya 16, iliyofanyiwa marekebisho 2022.

Inadaiwa kuwa, Gekul ambaye ni Mbunge wa Babati Mjini (CCM), alitekeleza tukio hilo tarehe 11 Novemba 2023, akiwa maeneo ya wilayani Babati na watu wengine ambao hawakuunganishwa katika kesi hiyo, ambapo alimlazimisha Ally avue nguo kisha akalie chupa iliyokuwa tupu, ili iingie katika sehemu zake za  kutolea haja kubwa, huku akimtishia kwa bastola.

Ally kupitia kwa wakili wake, Madeleka, aliamua kufungua kesi hiyo baada ya kuona upande wa Jamhuri unachelewa kuchukua hatua,  licha ya makundi mbalimbali ya watetezi wa haki za binadamu kupaza sauti wakitaka Gekul afikishwe mahakamani ili wajibishwe kama itabainika ana hatia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!