Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Malasusa: Kujilimbikiza mali, rushwa imerejea kwa kasi
Habari za SiasaTangulizi

Malasusa: Kujilimbikiza mali, rushwa imerejea kwa kasi

Spread the love

KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania limeonya watu kuacha tabia ya kujilimbikizia mali na kula rushwa kwa kuwa matendo hayo yamepigwa vita na Mungu. Anaripoti Faki Sosi…(endelea)

Akihutubia katika Misa takatifu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo leo tarehe 25 Desemba 2023 katika Kanisa la KKKT Azania Front jijini Dar es Salaam Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Alex Malasusa amewataka wakristo na Watanzania kuacha ubaya na tamaa za kidunia ikiwa pamoja na kula rushwa.

“Dunia imejaa ubaya na tamaa watu wamejaa tamaa katika dunia hii unapozungumzia rushwa na nimesikitika kusikia kwamba rushwa inaanza tena kukua kwa sababu rushwa ni roho yakutokuridhika, rushwa, dhulma na mambo mengine mengi yanayofanywa.”

“Paul anasema tuukatae  ubaya na tamaa za dunia sasa tuamue kuishi  kwa kiasi, ni kuishi kwa kuridhika”.

Amesema kuwa maandiko yapo wazi kuwa yanafundisha watu kutosheka.

“Nilikuwa najiuliza kwanini katika Sala  ile Bwana Yesu aliyotufundifa ‘Tupe leo riziki yetu tafsiri yake kamili utupe leo mkate wetu wa kila siku nikajiuliza kwanini hakutuambia utupe mikate yetu mpaka tutakapokufa kuna watu wanamikate mpaka ya vitukuu yaani anajaza hatosheki tunaambiwa tuishi kwa kiasi ” Amesema Malasusa.

Amesema kuwa hulka ya watu wasiotosheka ni kuwadhulumu wengine waliostahili na kwamba kama dunia ingekuwa ya haki tusengekuwa na masikini kiasi hiki lakini pia kama dunia ingekuwa na watu wenye huruma ingekuwa sehemu watu wanapopenda.

“Ukisikia mtu yoyote amekatisha uhai wake jiulize mchango wako ni nini wako watu wanakufa kwa sababu ya kukosa matibabu jiuze kwa sababu gani,” amehoji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!