Monday , 13 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rafat ajitosa kuwania uongozi chipukizi Taifa
Habari za Siasa

Rafat ajitosa kuwania uongozi chipukizi Taifa

Spread the love

Mtoto Rafat Ally Simba ambaye hivi karibuni alitikisa vyombo mbalimbali vya habari nchini baada kuandika na kuzindua kitabu chake cha The First Female President, (Rais wa Kwanza Mwanamke) sasa ameibukia Chama Cha Mapinduzi CCM na safari hii akiwania nafasi za Mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji Chipukizi Taifa Bara na Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mtoto Rafat Ally Simba

Kwa mujibu wa UVCCM, jina la Rafat mwenye miaka 11 ambaye pia mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji ya Chipukizi Tawi la Boko limerudi likiwa nafasi ya pili jambo linalomuhamasisha Mwanachipukizi huyo ambaye pia ni msemaji wa hadhara, yaani motivational public speaker, kutumia uwezo wake katika kuhamasisha watoto na vijana wenzake kujitambua, kujiamini na kupigania ndoto zao.

Kwa sasa Rafat Ally Simba ni mwanafunzi wa Darasa la sita katika shule ya Msingi Turkish Maarif iliyopo wilaya ya Kinondoni, Mkoani Dar es salaam akihudumu kama kiongozi mkuu wa wanafunzi shuleni hapo.

Kariba ya kiuongozi kwa mtoto Rafat ipo kwenye damu ambapo mbali na masomo binti huyo ni mwana mazingira, ambaye anaamini kuwa maisha ya usoni hasa kwa watoto yatategemea sana ni jinsi gani mazingira yanatunzwa kwa sasa.

“Hatuwezi kufikiria kuwa viongozi wa kesho iwapo kesho hiyo haitakuwa salama, hivyo nahamasisha vijana wenzagu kujitambua, kujiamini na kupigania ndoto zetu,” amesema mtoto Rafat Ally Simba.

Kwa upande wa lugha, Rafat anazungumza lugha tatu ikiwemo Kiswahili, Kiingereza na kifaransa emesema ufahamu wa lugha ni muhimu sana kwa kiongozi katika kuwasiliana na watu wake kwa ufasaha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!