Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mtanzania Joshua aliuawa na Hamas
Habari za SiasaTangulizi

Mtanzania Joshua aliuawa na Hamas

Spread the love

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema wamejulishwa na Serikali ya Israel kwamba Joshua Mollel, kijana wa Kitanzania aliyekuwa anasoma nchini humo, aliuawa baada ya kutekwa na kundi la Hamas tarehe 7 Oktoba 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Joshua alipoteza mawasiliano na ndugu zake ikiwamo Serikali ya Israel na Tanzania tangu tarehe 7 Oktoba 2023 yalipoibuka mashambulizi hayo huku serikali ya Tanzania ikifanya jitihada kubwa kupata taarifa zake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram leo Alhamis Makamba amesema “Nimeongea na Mzee Mollel, Baba mzazi wa Joshua, kuhusu ujumbe huo wa Serikali ya Israel, tunaendelea na mpango wa awali wa kuwapeleka Mzee Mollel na Mwanafamilia mwingine pamoja na Afisa wa Serikali nchini Israel, kuungana na Balozi wetu na Maafisa waliopo huko, kukutana na kuzungumza na mamlaka za Nchi hiyo ili kupata taarifa za ziada, kwa ridhaa ya Familia, na itakapobidi, tutatoa taarifa za ziada katika siku zijazo.”

Itakumbukwa tarehe 17 Novemba 2023 Serikali ya Tanzania ilitangaza kifo cha Clemence Felix Mtenga, Kijana Mtanzania ambaye alikuwa miongoni mwa Watanzania wawili ambao pamoja na raia wa Mataifa mengine hawakujulikana walipo tangu yaliyopotokea mapigano.

Waziri wa Nishati, January Makamba

Wizara ya mambo ya nje ilisema inaendelea kufuatilia taarifa za Mtanzania mwingine Joshua Mollel ambaye hakujulikana alipo tangu yalipotokea mashambulizi hayo.

Taarifa hiyo haikusema chanzo cha kifo cha Clemence lakini ilisema kijana huyo alikuwa ni miongoni mwa vijana wa Kitanzania wapatao 260 waliokwenda nchini Israel kushiriki mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vitendo chini ya Mpango wa Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Israel, ambapo baadaye mwili wa Clemence ulirejeshwa na Tanzania na kuzikwa tarehe 28 Novemba mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!