Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa UN kupiga kura ya dharura kusitisha vita Israel, Palestina
Kimataifa

UN kupiga kura ya dharura kusitisha vita Israel, Palestina

Spread the love

BARAZA Kuu la Umoja wa Mataifa (UN), leo tarehe 12 Disemba 2023, linatarajia kupiga kura ya dharura kuitaka Israel na kundi la wanamgambo wa Kipalestina, Hamas, kusitisha mapigano haraka iwezekanavyo kwenye Ukanda wa Gaza. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa….(endelea).

Uamuzi huo wa UN umerejewa tena baada ya ule ya kura ya awali iliyopangwa kupigwa katika baraza lake la usalama, kupingwa na Marekani.

Mtandao wa BBC Swahili umeripoti kuwa, kura ya sasa ni utekelezaji wa mapendekezo ya nchi za kiarabu na jumuiya ya ushirikiano wa kiislamu, yaliyoitaka UN iingilie kati ili vita hiyo iliyoanza mwanzoni mwa Oktoba 2023, imalizike.

Uamuzi huo wa UN unakuja baada ya vikosi vya jeshi vya Israel na Hamas, vikiendelea na mashambulizi kwenye ukanda huo.

Msemaji wa Jeshi la Israel, Avichay Adraee, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema Jeshi la Anga la Israel liemshambulia Gaza kwa kurusha makombora kadhaa ndani ya saa 24 zilizopita.

Wizara ya Afya ya Gaza, imedai wapalestina takribani 18,205 wameuwa huku 50,000 wakijeruhiwa tangu vita hiyo iliyodumu miezi miwili ianze.

Kwa upande wa Israel, watu zaidi ya 1,200 wameripotiwa kuuawa ikiwemo raia wa Israel na raia wa kigeni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Spread the loveAliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter...

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

error: Content is protected !!