Wednesday , 22 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mambo mawili yampeleka Mnyika Marekani
Habari za Siasa

Mambo mawili yampeleka Mnyika Marekani

John Mnyika
Spread the love

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, yuko nchini Marekani katika ziara ya kikazi ya siku nne, itakayoanza tarehe 4 hadi 7 Desemba 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa ya ziara hiyo  imetolewa jana tarehe 3 Desemba 2023 na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje Chadema, John Mrema.

Taarifa ya Mrema ilisema kuwa, Mnyika atafanya mambo mawili akiwa ziarani, la kwanza likiwa ni kuhudhuria jukwaa la mwaka la Vyama vya Kidemokrasia Duniani (IDU), lenye lengo la kujadili na kutoa msimamo juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani.

Jambo la pili ambalo Mnyika atalifanya katika ziara hiyo, ni kufanya majadiliano na mashirika mbalimbali ya kimataifa yenye makao makuu yake jijini Washngton, nchini humo.

“Katibu Mkuu ameondoka nchini  tarehe  3 Desemba 2023, alfajiri kuelekea nchini Marekani kwa ziara ya kikazi ya siku nne. Akiwa Jijini Washington, atahudhuria jukwaa la mwaka la IDU litakalohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa vyama na Serikali duniani,” ilisema taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yanawa mikono fidia Kimara-Kibamba

Spread the loveSERIKALI imewataka waathiriwa wa bomoabomoa ya upanuzi wa barabara ya...

Habari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

Habari za SiasaKimataifa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Habari za Siasa

Watumishi 85,471 walioenguliwa kipindi cha JPM wapandishwa vyeo

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa jumla...

error: Content is protected !!