CHAMA cha ACT Wazalendo kimeelezza kupokea kwa mshtuko na simanzi kubwa taarifa za vifo vya watu 47 na majeruhi 85 vilivyotokea wilayani Hanang mkoani Manyara kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu na Naibu Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo, Janeth Rithe imesema wanatoa pole na salaam za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa maafa haya makubwa yaliyotokea huku tukiwaombea kwa Mwenyezi Mungu majeruhi waweze kupona haraka na kuendelea na maisha yao ya kila siku.
Aidha, kutokana na maafa haya mazito, tunatoa wito kwa Serikali kuhakikisha majeruhi wanapata huduma zote stahiki zinazohitajika, huduma za kibinadamu kwa wakazi wote wa maeneo yaliyoathirika na maafa hayo sambamba na kukarabati miundombinu mbalimbali iliyoharibika kwa haraka zaidi.
Vifo hivyo na majeruhi hao wametokana na mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia jana Jumapili tarehe 3 Desemba 2023 baada ya sehemu ya Mlima Hanang kumomonyoka na kusababisha tope kutiririka katika makazi ya watu wa maeneo ya Katesh na Gendabi wilayani humo.
Leave a comment